Katibu wa Kamati ya kutetea haki za Waislamu,Sheikh Ponda Issa
Ponda(katikati) na wenzake 49 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu aliposomewa mashtaka ya uchochezi na kuvamia kiwanja kilichouzwa
na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) jijini Dar es salaam.
HATIMAYE washtakiwa wote katika kesi ya wizi na uchochezi
inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh
Ponda Issa Ponda wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Wakati washtakiwa hao wakipewa dhamana, Sheikh
Ponda ameendelea kubakia mahabusu kutokana na dhamana yake kufungwa na
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Dhamana kwa washtakiwa hao ilitolewa baada ya wote kutimiza masharti .
Dhamana kwa washtakiwa hao ilitolewa baada ya wote kutimiza masharti .
Miongoni mwa masharti hayo, ni kila mmoja kuwa na
wadhamini wawili wanaotambulika, wenye vitambulisho na wote kusaini
bondi ya dhamana ya Sh1 milioni.
Sambamba na masharti hayo, mahakama iliwapiga
marufuku washtakiwa hao kwenda eneo la mgogoro uliowasababishia kesi
hiyo (Markazi Chang’ombe) hadi kesi itakapokwisha.
Washtakiwa waliofikishwa mahakamani jana na
kuachiwa kwa dhamana ni 30, ambao waliungana na wenzao 19 ambao walikuwa
tayari wamepata dhamana kwa nyakati tofauti, baada kutimiza masharti
hayo.
Sheikh Ponda na wenzake 49 walipandishwa kizimbani
kwa mara ya kwanza Oktoba 18, mwaka huu chini ya ulinzi mkali na
kusomewa mashtaka matano yakiwamo wizi na uchochezi.
Tuhuma zingine ni kula njama, kuingia kwa nguvu
eneo lisilo mali yake kwa nia ya kutenda kosa, kujimilikisha ardhi kwa
nguvu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Mashtaka manne yanawahusu washtakiwa wote 50
isipokuwwa shtaka moja la uchochezi, ambalo linamhusu Sheikh Ponda pekee
anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya uhalifu.
Wakati kesi hiy ilipotajwa mahakamani hapo Novemba
Mosi, mahakama ilikubali kuwapa dhamana washtakiwa wote isipokuwa
Sheikh Ponda ambaye mahakama ilisema haina mamlaka ya kisheria kwa kuwa
DPP aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana yake.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hivyo, Kwaka aliomba mahakama ipange tarehe ya
usikilizaji wa awali (PH), washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali ya
kesi inayowakabili na kutakiwa kubainisha mambo wanayokubaliana na
wasiyokubaliana nayo.
Hata hivyo, Wakili wa washtakiwa hao, Juma Nassoro
alikumbusha mahakama kuhusu dhamana ya washtakiwa hao, akidai kuwa
wakati walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, maombi yao ya
dhamana hayakushughulikiwa kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi
hiyo hakuwapo.
Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi hayo ya
dhamana na kusema dhamana iko wazi kwa washtakiwa wote, isipokuwa Sheikh
Ponda ambaye dhamana yake imefungwa na DPP.

0 comments:
Post a Comment