BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKAZI BUNDA MKOANI MARA WAMLALAMIKIA RAIAS KIKWETE JUU YA KUKITHIRIN KWA VITENDO VYA RUSHWA NCHINI.

 
Rais Jakaya Kikwete.
  
Mwandishi Wetu, Bunda
WAKAZI  wa Jimbo la Bunda, katika Mkoa wa Mara wamesema kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini  ni matokeo ya ukimya wa Rais Jakaya Kikwete na kumwomba achukue hatua kudhibiti kwenye idara mbalimbali.

Wakitoa maoni yao wakati wa mdahalo wa kujadili uwajibikaji na uwazi wa watumishi wa umma, uliofanyika leo katika Mji mdogo wa Nyamuswa jimboni humo, wakazi hao walisema ukimya huo wa Rais unatoa mwanya kwa wasiowaadilifu kuifanya rushwa kama sheria maeneo ya kazini na hivyo kupotosha haki.

Walisema kama Rais Kikwete angewafuatilia wanaolalamikiwa na kuwatolewa uvivu hadharani ,  watumishi wengi wangepatwa na woga na hivyo kuacha  au kupunguza.

‘‘Kwa mfano, Rais angeonyesha mfano wa kumwajibisha Inspekta Jenerali wa Polisi  kutokana na idara ya polisi kuongoza kwa rushwa, bila shaka wakuu wa idara zingine wangesimama kidete kuzuia rushwa’’, walisema.

Mmoja wa wakazi hao, Charles Komanya alisema kukithiri kwa rushwa na ubinafsi miongoni mwa watumishi wa umma kumechangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa mfumo mzima wa haki katika jamii.

  “Ubinafsi na rushwa vimesababisha kudorora kwa haki katika
jamii. Watumishi na jamii kwa pamoja hawapati haki zao na hivyo
kupoteza kabisa uwazi na uwajibikaji nchini,”amesema Komanya.

Aidha wakazi hao pia waliviomba vyombo vinavyohusika na masuala ya kisheria kutoa elimu ya uraia kwa wananchi maana wengi wakiwamo watumishii wa Serikali ngazi za vijiji na kata wanaonekana kutokujua haki na wajibu wao hali inayopelekea wajanja wachache kutumia mwanya huo kujinufaisha kwa rushwa.

Mapema katika nasaha zake Katibu wa Mtandao wa ssasi za kiraia
wilayani humo (Bunda Ngonet) alisema watumishi wengi leo
hawawajibiki na kujituma kazini wala hawaonyeshi uzalendo kama
ilivyokuwa zamani na kuwataka watoe maoni yatakayoleta mabadiliko
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: