MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), amewafutia mashtaka watuhumiwa
watatu kati ya sita waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kutorosha
isivyo halali wanyamapori hai kwenda Doha, nchini Qatar.
Wanyama hao wakiwamo twiga wanne, wenye thamani ya
Dola 113,715 za Marekani walisafirishwa Novemba 26 mwaka kupitia Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo.
Ombi la kuwafutia mashtaka watuhumiwa hao liliwasilishwa mahakamani jana mjini Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Simon Kobelo.
Liliwasilishwa na jopo la mawakili watatu wa Serikali, Araffa Msafiri, Evetha Mushi na Pius Hilla.
Waliofutiwa mashtaka ni pamoja na Jane Mbogo, raia wa Kenya ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Equity Aviation Services na maofisa usalama wawili wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Authority (Kadco).
Maofisa hao ni Veronica Benno na Locken Kimaro ambao jopo la mawakili wa Serikali walisema DPP ameamua kuwafutia mashtaka na kuiomba mahakama iwaachie huru, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema chini ya kifungu
cha sheria kilichotumika kuwaondolea watu hao mashtaka, watuhumiwa
wanaweza kukamatwa tena na kushtakiwa kwa kosa hilo kama DPP ataona kuna
haja ya kufanya hivyo.
Katika hatua nyingine, upande wa mashtaka umebadilisha hati ya mashtaka, kusoma hati mpya na kumwongeza mshitakiwa.
Mshtakiwa huyo ni Michael Mrutu ambaye ni Ofisa
Usalama wa Kadco na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa waliobakia katika
kesi hiyo kuwa wanne.
Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande hadi Desemba 4
mwaka huu na kutakiwa kuwasilisha maombi yake ya dhamana katika Mahakama
Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, yenye uwezo wa kusikiliza mashtaka ya
uhujumu uchumi.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kamran
Ahamed ambaye ni raia wa Pakistan, Hawa Mang’unyuka, Mkurugenzi wa
Kampuni ya Osaka Traders na Martin Kimath ambaye ni Ofisa Mifugo wa
Shamba la Wanyama (Zoo Sanitary).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wote
wanne wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhujumu uchumi likiwamo la
kusafirisha wanyama kwenda Doha na kuisababishia Serikali hasara ya
Sh170.5 milioni.
Mshtakiwa Ahmed na Hawa wanakabiliwa na mashtaka mengine yakiwamo ya kula njama na kufadhili utoroshwaji wa wanyama hao, kufanya biashara ya wanyamapori bila leseni na kumiliki nyara za Serikali isivyo halali.

Kwa upande wao, Kimath na Mrutu wanakabiliwa na
mashtaka ya kuwezesha kufanikisha mpango wa kuwatorosha wanyama hao,
kushindwa kuzuia kosa na pia kushindwa kutoa taarifa za tukio hilo.
Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao.
Hata hivyo, washtakiwa walikanusha mashtaka dhidi yao.
Jopo la mawakili wanaoendesha kesi hiyo waliiambia
mahakama kuwa upelelezi umekamilika na kwamba jana walikuwa tayari
kuanza usikilizaji wa awali.
Hata hivyo washtakiwa waliiomba mahakama iahirishe kuendelea na usikilizaji huo wa awali, kwa maelezo kuwa wanatarajia kukodi mawakili wa kuwatetea na hasa ikizingatiwa kuwa wao hawajui sheria zinazohusu kosa linalowakabili.

Hakimu Kobelo alilikubali ombi hilo na kuahirisha
kesi hiyo hadi Desemba 4 mwaka huu na kuwataka washtakiwa wahakikishe
siku hiyo wanakwenda na mawakili wao, ili mahakama ipange tarehe ya
usikilizaji wa awali.

0 comments:
Post a Comment