
Aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Urusi Anatoly Serdyukov kataka midotcomnewsindonesia.wordpress.com.
Putin ameziba pengo la waziri Anatoly Serdyukov ambaye amekuwa akitekeleza mageuzi ya kijeshi yasiyo maarufu ingawa yaliungwa mkono na chama cha Kemlin kwa kumpa nafasi hiyo gavana wa zamani wa jimbo la Moscow na waziri wa mambo ya dharura Sergei Shoigu.
Wachambuzi wanasema kwamba kufutwa kazi kwa afisa huyo wa juu ambaye amenufaika na uungwaji mkono usio na masharti wa rais Putin ni hatua inayolenga kuwatia hofu wasomi wakati rais huyo anapo pambana na mgogoro mbaya wa kisiasa katika miaka takriban 13 ya uongozi wake.
Putin aamesema kuwa Serdyukov, mmoja wa watu watatu nchini Urusi wenye uwezo wa kupata namba ya kianzio ya uzinduzi wa nyuklia, ameondolewa katika wadhifa wake ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa ya dola.

0 comments:
Post a Comment