BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK KIGODA: TUTAIPUNGUZA BEI YA UMEME VIWANDANI.



Dk Abdallah Kigoda.
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema atapambana kuhakikisha viwanda vinapunguziwa bei ya umeme ili kuleta ufanisi wa uzalishaJi wa bidhaa.
Amesema hayo wakati Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) tayari limewasilisha kwa Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura) maombi ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 150 ifikapo Januari mwakani.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), jijini Dar es Salaam jana, Dk Kigoda alisema kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wataangalia tozo za gharama za umeme kwa viwanda nchini.
Alisema mpango huo wa kupunguza gharama za umeme zinalenga kuviwezesha viwanda kuzalisha kiwango cha juu ukilinganisha na sasa.
“Viwanda vinaweza kufanya vizuri endapo nishati hiyo itapatikana kwa uhakika kwani bila hivyo itakuwa ngumu kuzalisha bidhaa nyingi na bora,” alisema Dk Kigoda na kuongeza:
“Mfano unaangalia katika kiwanda kimoja, asilimia 40 ya mapato wanatumia kulipia gharama ya umeme, lakini ikiwa watatumia asilimia 20 kiwanda kitazalisha kwa urahisi na bei itapungua,” alisema.
Dk Kigoda alisema suala la bidhaa zisizo na ubora hapa nchini limeendelea kushamiri na hivi sasa limefikia asilimia 20 ya bidhaa zote zinazouzwa sokoni.
“Ninyi CTI mtakuwa mnawajua wafanyabiashara wanaiongiza bidhaa bandia hivyo tunaomba muwataje ili waweze kuchukuliwa hatua sitahiki,” alilalamika Dk Kigoda.
Naye, Mwwenyikiti wa CTI, Felix Mosha alisema suala la bidhaa bandia kuwepo sokoni linatokana na Serikali kutokutekeleza kwa vitendo ukaguzi wa bidhaa kabla hazijaingia nchini.
“Serikali inatakiwa kutekeleza kwa vitendo ukaguzi wa bidhaa kabla hazijaingia nchini. Hii itasaidia kuhakikisha haziingii katika masoko,” alisema Mosha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: