BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KENYETTA NA RUTO WAUNDA TIMU RASMI KATIKA MBIO ZA UCHAGUZI MKUU 2013 KENYA.

Kenyatta na Ruto

WANASIASA wawili wa Kenya wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.


Katika mkutano wa hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea mwenza wa Bwana Kenyatta.

Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka.

Wanasiasa wengine maarufu wa Kenya piya wameshtakiwa na ICC.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: