KUNDI la wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira,
wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilayani Rufiji na kufanya vurugu kubwa
baada ya raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kipigo cha Polisi.
Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinaipasha
kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo hicho ni Hamis Mpondi, ambaye mauti
yamemfika wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili.
Habari zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao
wanaendelea kuteketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo
hicho, licha ya Polisi kuendelea kufanya juhudi za kuwatawanya kwa mabomu
katika eneo hilo.
Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya
Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma
matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa
Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu
hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu. Vurugu zinaendelea, Habari
kwa hisani ya Father Kidevu.
0 comments:
Post a Comment