MEZA yetu ya habari
imepokea taarifa fupi toka Mtwara usiku wa kuamkia leo ikitujuza kuchomwa
moto kwa gari moja linalosadikiwa kutumika kwa biashara ya abiria
(TAX) huko Mtwara.
Chanzo chetu kimeelezwa
kuwa mkasa huo unapewa mahusiano na sakata la GESI linaloendelea hivi sasa
hapa nchini kwani gari hiyo inasemekana lilitaka kumtorosha Bibi mmoja
mkazi wa kijiji cha Msimbati-Mtwara aliyetoa ahadi kuwa gesi ikisafirishwa
kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam kama serikali ilivyokusudia basi itageuka
kuwa Maji na si gesi tena.
Inasemekana bibi huyo
alitaka kwenda kuonana na wazee wa kimila
na kuongea na kuhusu suala zima la gesi, bado haijafahamika nini
bibi huyo alitaka kujadili na wazee hao wa kimila.
Hadi sasa
haijajulikana nani kahusika na tukio hilo na haijajulikana kama kuna watu
wameumia kutokana na tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment