BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAZI YA KUTULIZA GHASIA ZA MAANDAMANO ILIVYOKUWA KWA WANAFUNZI WA IFM KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM.


Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka!
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko. 
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu. 
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
Askari Polisi ambaye hakuwa kwenye sale za jeshi hilo akimsulubu mmoja wa wanafunzi wa IFM baada ya kudhibitiwa kwenye eneo la kituo cha Polisi Kigamboni walipofika kutaka kulazimisha kufanyika mkutano wao na kamanda Kova badala ya eneo lililopangwa kwenye viwanja vya Machava. Wanafunzi hao walikamatwa baada ya kupigwa mabomu ya machozi kwenye eneo hilo na kukamatwa kama kuku wa mdondo.
Askari wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa chuo cha IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi.
Kundi la wanafunzi walishikwa kama kuku wa mdondo baada ya kupigwa mabomu ya machozi na kujikuta wakijificha sehemu moja kundi zima hali iliyosabisha kutembezwa kichurachura hadi kwenye kituo cha Polisi cha Kigamboni.
Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi.
Mwanafunzi huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni.
Baada ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako walijificha wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi ili wajisalimishe.
Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga.
Hapa amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini.
Huyu hakujiweza kabisa mabomu yalimchanganya na kudondoka toka kwenye Difenda ya Polisi.
Virungu vilitumika kushindilia watu kwenye Difenda.
Hiki ndicho kikosi Kamili kilichotumia dakika 15 kusambaratisha kundi la wanafunzi zaidi ya 800 walioweka kambi ya muda mfupi kwenye kituo cha Polisi Kigamboni.
http://kajunason.blogspot.com/
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: