BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE YA ATCL YAKAMILIKA UTENGENEZAJI WA KIOO, YAANZA SAFARI MKOA WA KIGOMA.

ATCL 3

Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog.

ATCL 1Marubani   wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo asubuhi. Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
ATCL 2Kapteni  Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8 Q300 .Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22. Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.


Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: