Vijana wa kimasai jamii ya wafugaji (Morani) kutoka vijiji vya wafugaji zaidi ya vitano wakisikiliza viongozi wa jamii hiyo wakati wa kikao cha pamoja cha wafugaji cha kujadili tamko la halmashauri la kutaka kufanyika kwa operesheni ya kuwaondoa wafugaji wageni kilichofanyika katika kijiji cha Twatwatwa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.
Mchungaji wa kanisa la Calvary Assemblies of God kijiji cha Parakwiyo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Ibrahim Oloishuro akifafanua jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wafugaji wa kujadili waraka wa
serikali wakutaka kufanya operesheni ya kuwaondoa wafugaji wavamizi
wanaodaiwa kutokea katika wilaya za Ulanga na Kilombero wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.
MAHAKAMA KUU TANZANIA YAZUIA KUFANYIKA KWA OPERESHENI KUWAONDOA WAFUGAJI WAGENI KILOSA.
MAHAKAMA Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imetoa zuio la kusudio la wilaya ya Kilosa la kufanyika operesheni ya kuwaondoa wafugaji wageni katika sehemu mbalimbali za wilaya hiyo hadi pande mbili za walalamikiwa na washkatiwa zitapokutana kwa ajili ya majadiliano Januari 13 mwaka huu katika mahakam hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Morogoro mmoja wa wafugaji waliofungua
kesi hiyo, Paul
Sauyaki alisema kuwa mahakama kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio la
kufanyika kwa operesheni ya kuwaondoa wafugaji wageni ndani ya wilaya ya Kilosa hadi pande mbili zitakapokaa na kubainisha wageni wa namna gani wataondolewa kwenye
opeeresheni hiyo.
Sauyaki alisema kuwa lengo la kwenda mahakama kuu Tanzania kufungua kesi
hiyo imetokana na kasoro nyingi zilizojitokeza katika operesheni ya mwaka 20009
ambapo wafugaji 74 ambao walipoteza mifugo
wakiwemo ng’ombe 8708, mbuzi 1536 na kondoo 144 na kufanya idadi ya mifugo
iliyopotea katika operesheni hiyo kufikia 10,338 wamefungua kesi dhidi ya halmashauri
kudai fidia.
“Katika ile operesheni ya mwaka 2009 tayari wafugaji 74 wamefungua
kesi mahakamani kudai fidia kutokana na mifugo yao kuporwa na watendaji
waliokuwa wakiendesha operesheni zaidi ya 10, 300 sasa hali kama hiyo
hatutaweza itukute tena mwaka huu ndiyo maana tumefungua kesi mahakama kuu
tanzani kwa lengo la kuzuia mpaka pande mbili zikutane. Alisema Sauyaki.
Kuna mapungufu mengi yamekuwa yakifanyika katika operesheni za kuwaondoa
wafugaji moja ya mapungufu hayo ni kwa baadhi ya watendaji
kuwatesa wafugaji, kuporwa mifugo na familia za
jamii ya wafugaji kuishi kwa hofu
kutokana na vitisho vinavyodaiwa kutolewa na baadhi ya watendaji hao.
Kesi hiyo ambayo ipo chini ya wakili, Barnabas Luguwa yenye no1/2013 ikiwa na waombaji wanne akiwemo
Israel kilwaha, Ibrahim Oloishulo, Julius Meglory na Paul Sauyati kwa niaba ya wafugaji 112 walalamikiwa ikiwa ni mkuu wa wilaya Kilosa, Mwanasheria mkuu na Halmashauri
ya wilaya.
Pande
hizo zinatarajia kukutana katika mahakama hiyo januari 13 mwaka huu majira ya saa 4.00 asubuhi jijini Dar es
Salaam.
Naye mkuu
wa mila wa jamii ya wafugaji wilaya hiyo (LEGWENANI) Kilindi Lestino
amepongeza hatua ya mahakama kuu Tanzania kutoa zuio hilo kwani itasaidia pande mbili hizo
kusaidia kupata makubaliano yatayosaidia kuondoa kasoro zilizojitokeza katika
operesheni ya mwaka 2009.
Lestino
alisema kuwa baada ya kufanyika kwa operesheni ya mwaka 2009 jamii hiyo ya wafugaji wamejikuta wakihudumia zaidi ya kaya 200 za wafugaji ambao waliathirika na operesheni
hiyo kutokana na kupoteza mifugo zaidi ya 20,000 wakiwemo ng'ombe, mbuzi na kondoo ambao
tangu kipindi hicho wamekuwa wakiishi katika mazingira ya umasikini kutokana na kukosa
chakula kikuu kinachotokana na mifugo hiyo kwa ajili ya kukamua maziwa.
Mmoja wa v iongozi wa jamii ya wafugaji wilaya ya Kilosa Adam Mwarabu akieleza jambo katika mkutano huo huku mwandishi wa ITV mkoa wa Morogoro Devotha Minja akichukua picha kwa ajili ya kurusha katika chombo chayo.
Katibu wa chama cha ushirika kijiji cha Mbwade, Paul Sauyaki wakati wa mkutano wa wafugaji wa kujadili waraka wa serikali wakutaka kufanya operesheni ya kuwaondoa wafugaji wavamizi wanaodaiwa kutokea katika wilaya za Ulanga na Kilombero wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.
Sehemu ya wafugaji wa vijiji mbalimbali wakisikiza viongozi wao wakati wa mkutano wa wafugaji wa kujadili waraka wa serikali wakutaka kufanya operesheni ya kuwaondoa wafugaji wavamizi wanaodaiwa kutokea katika wilaya za Ulanga na Kilombero wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro.
WAFUGAJI WA JAMII YA KIMASAI KILOSA WAITAKA SERIKALI KUWASHIRIK ISHA KATIKA OPERESHENI ZIKINEVYO DAMU ITAMWAGIKA .
VIONGOZI
wa jamii ya wafugaji wa kimasai wamekuwa katika wakati mgumu wa kuwatuliza
vijana wa kimasai (Moran) wakidaiwa kufanya mazoezi ya kupambana na askari
wataoendesha operesheni ya kuwaondoa wafugaji waliovamia wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro.
Wakizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wafugaji katika
kijiji cha Mbwande wilayani humo mmoja wa viongozi hao Katibu wa chama cha
ushirika kijiji chicho, Paul Sauyaki alisema kuwa kwa sasa viongozi wa mila wa
jamii hiyo ya jamii ya kimasai wapo katika wakati mgumu wa kutuliza hasira za
morani ambao wanadaiwa kutaka kupambana na watendaji wataoendesha operesheni ya
kuwaondoa wafugaji waliovamia wilayani humo itayoanza hivi karibuni.
Sauyaki
alisema kuwa viongozi ndani ya jamii hiyo wapo katika kutafuta mbinu ya
kuwatuliza hasira na jazba baada ya kupata waraka wa serikali wa Kilosa
kufuatia kutoa siku 10 ya kuwasaka na kuwaondoa wafugaji wanaodaiwa kuvamizi
sehemu mbalimbali za vijiji vya wilaya hiyo na mifugo yao wakitokea katika
wilaya ya Kilombero na Ulanga ambapo kuna operesheni ya kuwaondoa wafugaji
katika bonde la Kilombero.
“Tupo
katika wakati mgumu sana sisi viongozi wa wamasai kwa sasa na hii inatokana na
morani kutaka kuwadhuru watendaji wataoondesha operesheni ya kuwaondoa wafugaji
waliovamia Kilosa ikiwa seehemu ya kupinga waraka wa siku 10 wa serikali wa
kuwaondoa wafugaji wavamizi wanadao daiwa kutokea Kilombero na Ulanga ambako
nako kuna operesheni ya kuwaondoa wafugaji waliovamia hifadhi ya bonde la mto
Kilombero. Alisema Sauyaki.
Mchungaji
wa Kanisa la Calvary Israel Kilwaha alisema kuwa kuibuka kwa migogoro mingi
katika wilaya hiyo baina ya wafugaji, wakulima na wawekazi hivi sasa
kumesababishwa na serikali yenyewe baada ya wafugaji kukosa sehemu za kulishia
mifugo jambo ambalo limesabaisha kuwa na migogoro mingi.
Kilwaha
alisema kuwa endapo serikali ya wilaya ya Kilosa isingetoa ranchi kwa wawekeza
wa nje ingepunguza migogoro kwa kutoa maeneo ranchi hizo kwa wafugaji wenyeji.
“Ukiangali
kwa umakini utaona kuwa serikali imekuwa ikifanya mambo mengi biloa
kushirikisha wahusika katika mambo mbalimbali lakini kwa upande wa wafugaji
hizi ranchi zilizotelekezwa na Nafco wangepewa wafugaji wenyeji lakini badala
yake serikali hiyo hiyo yennye lengo la kutatua migogoro imetoa ranchi kwa
wawekezaji wageni sasa hapo migogoro itaisha ? alihoji Mchungaji Israel.
Aliendelea
kusema kuwa kwa serikali kutoa ranchi kwa wawekezaji wa nje kunachangia kwa
kiasi kikubwa cha migogoro kwani wangeweza kutoa kwa wafugaji wenyeji ambao
wana uwezo wa kuzinunua huku wawekezaji hao wakidaiwa kutoziendeleza.
Isarael
alisema kuwa hasira za morani zinatokana na kukumbuka upotevu wa mifugo wakati
wa operesheni ya mwaka 2009 iliwakumba wafugaji wenyeji na wavamizi jambo
ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu inadaiwa wafugaji wengi walipata harasa kwa
madai mifugo yao kutaivishwa jambo ambalo hawataweza kuona hali hiyo ikijitokea
tena katika operesheni hiyo.
Akizungumzia
malalamiko hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Amer
Mbaraka alisema kuwa oparation hiyo inalenga kuwaondoa wafugaji wavamizi
waliotoka wilayani Kilombero na Ulanga ambao wanadaiwa kuingia katika wilaya
hiyo na kuwa oepereasheni hiyo haitawaathiri wa fugaji halali wa wilaya
ya kilosa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya serikali ya wilaya ya Kilosa kutoka notisi ya siku 10
kuanzia dec 2012 ambapo leo (jana) ilitarajiwa kuanza kwa operesheni hiyo.
Katika
mkutano huo pia kuliibuka machungu ya oparation ya mwaka 2009 ambapo
walikumbushia baadhi ya fedha zilizokusanywa kushindwa kurudi kwa kunufaisha
wafugaji kama ilivyoagizwa na serikali.
0 comments:
Post a Comment