BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KILELE CHA MIAKA 50 YA UTANGAZAJI LA UJERUMANI DW YAANZA KUADHIMISHWA.

Kiswahili Redaktion DW Gruppenbild
***
eingestellt im Januar 2013 
SHIRIKA la kimataifa la Utangazaji la Ujerumani DW, limeanzisha sherehe ya miaka 50 tangu lilipoanzisha shughuli zake likisikika Afrika Mashariki na Kati, sherehe ambazo zitahitimishwa ijumaa kwa mdahalo maalumu.

Mkuu wa idhaa hii, Andrea Schmidt akiwa  na baadhi ya wafanyakazi, alikuwa na mkutano na waandishi wa habari, mkutano ambao umehudhuriwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes, ambao wote kwa pamoja wamejadili nafasi ya vyombo vya habari kwenye ujenzi wa jamii imara.

Maadhimisho hayo yanafanyika sambamba na mdahalo maalumu ulipangwa kufanyika siku ya ijumaa ukuwaleta pamoja magwiji wa uandishi wa habari pamoja na wanaharakati wa maendeleo. 

Mada mbalimbali kuwasilishwa
Mohamed Abdulahman.
Januar, 2013, Bonn  
MKUU wa Idhaa ya Kiswahili Andrea Schmidt wakati alipokuwa na watangazaji wa Zenj FM mjini Unguja.
 
Chini ya maudhui isemayo "Maarifa na Mwamko" watoa mada kwenye mjadala huo wanatazamia kujadilia kwa kina nafasi ya vyombo vya habari katika ujenzi wa jamii bora na ukuzaji wa masuala ya haki za binadamu na demokrasia. 

Hatua ambayo itatanguliwa na hotuba maalum kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili DW, Andrea Schmidt.

DW ambayo ilianza kupeperusha matangazao yake miaka 50 iliyopita wakati wa vugu vugu la vita baridi, inajivunia mafanikio iliyoyopata katika eneo la afrika mashairiki na kati na hata maeneo mengine duniani yanayozungumza lugha ya Kiswahili.

Kiswahili kimekuwa duniani
Der Journalist Mohamed Abdulahman.
Januar, 2013, Bonn  
Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Mohamed Abdulrahman.
 
Akizungumzia hatua ya DW kuadhimisha sherehe hizi nchini Tanzania, Naibu Mkuu wa idhaa ya Kiswahili Mohamed Abdulrahman alielezea sababu za maadhimisho hayo kufanyika Dar es Salaam. 

"Kwanza tunawasikilizaji wengi Tanzania. Tanzania tunaweza kusema ni chimbuko la lugha ya Kiswahili, nia vilevile imefanya mengi katika kukiendeleza Kiswahili na kufikia hatua ambayo hii leo lugha hiyo sio tu kwamba inazunguzwa katika nchi ambazo zinazungumza katika eneo hilo la Afrika maashariki na Kati.

Kinazungumzwa hata katia nchi za Ulaya kwa maana ya kwamba vyuo vikuu takriabani vyote barani Ulaya na Marekani kwa sehemu fulani vina idara mbalimbali za lugha na miongoni mwa lugha hizo ni Kiswahili". Alisema mtangazaji huyo mkongwe.

DW ambayo huendeshwa kwa bajeti ya serikali ya Ujerumani
inakusanya jumla ya wafanyakazi 1,500 waliogawika katika vitengo mbalimbali na katima msimu wa mwaka ulipita alipata kiasi cha euro milioni 270 kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za utangazaji duniani kote. 

Balozi asisitiza uhuru wa habari
Akizungumzia kuhusu uhuru wa vyombo vya habari kwa nchi za Afrika, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus Peter Brandes alisema kuwa nchi za Umoja wa Ulaya zinapendelea kuona uhuru huo unaheshimika. 

Alisema kuwa Umoja wa Ulaya ambayo moja ya nguzu yake muhimu na kusimamia haki za binadamu na uhuru wa Maoni, hivyo Ujerumani ikiwe sehemu ya Umoja huo itaendelea kutilia mkazo umuhumu wa kuheshimiwa uhuru huo wa maoni. 

Uhuru wa vyombo vya habari ni moja ya nguzo muhimu kunapotajwa dhana ya maendeleo na ukuaji wa demokrasia
Mwishoni mwa mdahalo huo washiriki watapa fursa ya kujadiliana haya na yale kuhusiana na utendaji wa vyombo vya habari. 
Sikiliza taarifa ya George Njogopa kutoka Dar es Salalaam. 

Sikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: