Askari wa Nigeria huko Ibadan.
Rais wa Ufransa, Francois Hollande akitoa hotuba huko Paris juu ya operesheni za kijeshi za nchi hiyo.
MAAFISA wa Nigeria wanasema utafutaji unaendelea kwa maharamia wanaodai
dola milioni 1.3 kwa raia wa nje sita waliotekwa kutoka kwenye meli
Jumapili.
Msemaji wa Polisi huko katika jimbo la Bayelsa amesema Jumatano kuwa mmoja kati ya washukiwa watekaji aliwapigia maafisa kudai malip hayo ili kuwaachia mateka hao.
Amesema watatu kati ya wafanyakazi waliotekwa ni kutoka Ukraine, wawili kutoka India na mmoja kutoka Russia.
Raia hao wa nje walichukuliwa mateka baada ya maharamia kushambulia meli yao kwenye pwani ya Nigeria.
Meli hiyo inamilikiwa na Century
Group shirika lenye makao yake Nigeria la mafuta .
0 comments:
Post a Comment