“ Niliomba mwenyewe kuondoka, niliwaeleza kuwa
nisingependa kuendelea tena kuongoza baraza hilo nina mambo mengine ya
kufanya, nilikuwa na ndoto za kuwafikisha mahali.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alisema amekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kwa miaka 15 na kwamba ameliongoza kwa mafanikio.
“ Niliomba mwenyewe kuondoka, niliwaeleza kuwa nisingependa kuendelea tena kuongoza baraza hilo nina mambo mengine ya kufanya, nilikuwa na ndoto za kuwafikisha mahali ambapo wanaweza kujitegemea, mwisho wanihesabu kuwa mimi ni mtumishi nisiye na faida, nimefanya yale yaliyonipasa, nimefanikiwa,” alisema Lowassa.
“Mafanikio makubwa ni pamoja na kuwawezesha vijana kujitegemea, kwa kuweza kumiliki jengo la uwekezaji, kwa fedha wanazozipata huko wanaweza kujilipa mishahara yao wenyewe, ni mradi mkubwa ambao hata chama chenyewe hakina,” alisisitiza.
“Ninajivunia mafanikio yaliyopatikana, chini ya uongozi wangu baraza limeweza kufanya kazi nzuri…Ninawapongeza kwa hayo, pia ninawashukuru vijana kwa kuniamini na kunipa nafasi kwa miaka yote hiyo,” alisema Lowassa.
Juzi Katibu wa UVCCM, Martin Shigela alitangaza kuchaguliwa kwa viongozi wapya wa baraza hilo na nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Lowassa ilichukuliwa na Dk Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Jengo ambalo anajivunia Lowassa liliwahi kuzusha mtafaruku ndani ya UVCCM na kusababisha Nape Nnauye kuvuliwa uanachama wa umoja huo, baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma mbalimbali alizozitoa kuhusu mradi wa jengo hilo akieleza kuwa kuna ufisadi.
Nape alidaiwa kusema uongo kuhusu mradi huo wa jengo la UVCCM akiwatuhumu viongozi wa jumuiya hiyo hadharani na nje ya vikao, ambapo ilielezwa kwa kufanya hivyo alikuwa kinyume na kanuni za 17 (C) na18 (B) za umoja huo.
WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU EDWARD LOWASA.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ametamba kuwa
anajisikia furaha kwa kutimiza ndoto yake ya kuujengea uwezo, Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, (UVCCM), ndiyo maana akaomba asichaguliwe
tena kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Udhamini la umoja huo.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, alisema amekuwa mwenyekiti wa baraza hilo kwa miaka 15 na kwamba ameliongoza kwa mafanikio.
“ Niliomba mwenyewe kuondoka, niliwaeleza kuwa nisingependa kuendelea tena kuongoza baraza hilo nina mambo mengine ya kufanya, nilikuwa na ndoto za kuwafikisha mahali ambapo wanaweza kujitegemea, mwisho wanihesabu kuwa mimi ni mtumishi nisiye na faida, nimefanya yale yaliyonipasa, nimefanikiwa,” alisema Lowassa.
“Mafanikio makubwa ni pamoja na kuwawezesha vijana kujitegemea, kwa kuweza kumiliki jengo la uwekezaji, kwa fedha wanazozipata huko wanaweza kujilipa mishahara yao wenyewe, ni mradi mkubwa ambao hata chama chenyewe hakina,” alisisitiza.
“Ninajivunia mafanikio yaliyopatikana, chini ya uongozi wangu baraza limeweza kufanya kazi nzuri…Ninawapongeza kwa hayo, pia ninawashukuru vijana kwa kuniamini na kunipa nafasi kwa miaka yote hiyo,” alisema Lowassa.
Juzi Katibu wa UVCCM, Martin Shigela alitangaza kuchaguliwa kwa viongozi wapya wa baraza hilo na nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Lowassa ilichukuliwa na Dk Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Jengo ambalo anajivunia Lowassa liliwahi kuzusha mtafaruku ndani ya UVCCM na kusababisha Nape Nnauye kuvuliwa uanachama wa umoja huo, baada ya kushindwa kuthibitisha tuhuma mbalimbali alizozitoa kuhusu mradi wa jengo hilo akieleza kuwa kuna ufisadi.
Nape alidaiwa kusema uongo kuhusu mradi huo wa jengo la UVCCM akiwatuhumu viongozi wa jumuiya hiyo hadharani na nje ya vikao, ambapo ilielezwa kwa kufanya hivyo alikuwa kinyume na kanuni za 17 (C) na18 (B) za umoja huo.
0 comments:
Post a Comment