BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKUBALIANO YA AMANI YA DRC YATIWA SAINI

 Rais wa DRC, Joseph Kabila
 RAIS KABILA.United Nations Secretary-General Ban Ki-moon, center, joins hands with President of the Democratic Congo Joseph Kabila Kabange, left, and President of Rwanda Paul Kagame at the 67th session of the General Assembly at United Nations Headquarters, Sept. 27,
KATIBU Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon katikati akiwa na marais wa Ruanda kulia, Poul Kagame na Joseph Kabila wa Congo DRC.
 
BAADHI ya viongozi wa kikanda  barani Afrika  wametia saini makubaliano yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa Jumapili, kwa lengo la kumaliza mtafaruku wa miongo miwili katika eneo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Makubaliano hayo yametiwa saini  katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. 
 
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alihudhuria sherehe hizo pia na kusema makubaliano hayo ni mwanzo wa  mchakato wa kufikia maelewano ya kudumu.

Inategemewa makubaliano hayo pia yatakuwa chanzo cha kuunda kikosi cha kikanda  kupambana na waasi katika eneo hilo lenye utajiri wa madini la DRC mashariki.

Viongozi hao wa Afrika walitegemewa kutia saini makubaliano hayo mwezi jana lakini yakaahirishwa baada ya kuibuka wasiwasi juu ya nani atakayeoongoza kikosi hicho cha kikanda.

Viongozi wa ukanda wa maziwa makuu  watakutana tena Kampala, Uganda Machi 15 kuendelea na majadiliano ya kusuluhisha mzozo baina ya serikali ya Kinshasa na kundi la waasi wa M23.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: