Kwa ufupi.
Tofauti na kanuni yake, leo Benedict hatavaa viatu
vyekundu kama ilivyozoeleka na badala yake amechagua viatu rahisi vya
ngozi vilivyobuniwa Mexico.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz
Baba Mtakatifu Benedict XVI.
YAMETIMIA.
SAFARI ya miaka saba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI inakamilika leo pale atakapong’atuka rasmi katika uongozi wa Kanisa Katoliki, ifikapo saa 2:00 usiku kwa saa za Italia (saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania).
SAFARI ya miaka saba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI inakamilika leo pale atakapong’atuka rasmi katika uongozi wa Kanisa Katoliki, ifikapo saa 2:00 usiku kwa saa za Italia (saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania).
Kwa siku mbili, Papa amekuwa na shughuli nyingi katika makao yake, Gandolfo Castel, Vatican akijiandaa kimwili kuondoka, akiweka sawa nyaraka zake binafsi na zile za kanisa ambazo zitawekwa katika kumbukumbu.
Kwa upande mwingine Vatican, nchi ambayo ipo ndani ya Jiji la Rome iliyozungukwa na ukuta, ikiwa na ukubwa wa hekta 44 na wakazi 832 pekee, imekuwa katika hekaheka nyingi.
Jana, waumini zaidi ya 50,000 na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwamo makardinali, maaskofu, mapadri na walei walialikwa kwa shughuli rasmi ya kumuaga kiongozi huyo.
Tofauti na kanuni yake, leo Benedict hatavaa viatu vyekundu kama ilivyozoeleka na badala yake amechagua viatu rahisi vya ngozi vilivyobuniwa Mexico. Alipewa viatu hivyo ikiwa ni zawadi wakati wa ziara nchini humo 2012.
Tangu alipotangaza uamuzi wake wa kung’atuka Februari 11, mwaka huu, utata umegubika nafasi yake katika maisha mapya ndani ya Vatican, akiitwa Papa Mstaafu.
Waumini, wataalamu na hata viongozi mbalimbali wa Kikatoliki wameanza kuhoji ni jinsi gani viongozi wawili (Papa) wataishi, huku wote wakivaa mavazi meupe wakiitwa Papa, wakiishi umbali mdogo kati yao, wakiwa na wasaidizi wengi wanaowahudumia.
Vatican.
Nje ya Gandolfo Castel, ulinzi umeimarishwa na vibali vya kuingia Vatican vimesitishwa.
Juzi, Vatican ilitangaza kwamba Papa Benedict XVI atajulikana kama ‘Emeritus Pope’, yaani Papa Mstaafu mwenye cheo cha heshima, akiendelea kuitwa, ‘mtakatifu’ na ambaye ataendelea kuvaa nguo nyeupe.
Mavazi na hata jina lake jipya ni masuala ambayo yamezua uvumi mwingi, huku suala la mrithi wake mpya pia likiwa gumzo, kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 600 iliyopita.
Ni uamuzi uliolishtua kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni duniani na wengi wanasema awali, haikushauriwa Papa kustaafu kwani kwa kufanya hivyo kunaacha mizozo na minong’ono ya kuwania madaraka.
Hata hivyo, uongozi wa Vatican umesisitiza kuwa uamuzi huo wa Papa Benedict XVI ni wa kipekee na hakuna mzozo ambao utatokea baina yake na mrithi wake ambaye mchakato wa kumpata unatarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.
“Kulingana na mabadiliko katika kanisa letu, kuna Papa mmoja. Ni dhahiri kwamba katika hali ya sasa hakutakuwa na tatizo,” anasema Mhariri wa Gazeti la L’Oservatore Romano linalomilikiwa na Vatican, Giovanni Maria Vian.
Hofu iliyopo.
Hata hivyo, wakosoaji wa mambo hawakubaliani na hoja hiyo na baadhi ya makardinali walioko Vatican kwa usiri mwingi, wanazungumzia suala hilo wakieleza kwamba litazua tatizo kubwa kwa Papa ajaye, hasa ikiwa mtangulizi wake, Benedict akiwa bado hai.
Mtaalamu wa tauhidi (theolojia), raia wa Uswisi, Hans Kueng ambaye amekuwa mtu wa karibu wa Papa Benedict XVI, ingawa kwa sasa ni mkosoaji wake amesema.
“Kwa sasa, Benedict XVI akiwa bado hai, kuna hatari ya kuwa na Papa kivuli, mwenye mamlaka kamili ambaye kwa chinichini anaweza kumshinikiza mrithi wake kufikia uamuzi.”
Hans Kueng alisema hayo alipozungumza na Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani.
Msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi alisema Papa Benedict XVI kwa upande wake aliamua aitwe Papa Mstaafu au ‘kiongozi mstaafu wa Roma.’
Anasema haelewi ni kwa nini ameamua kuacha jina lake la sasa la Askofu wa Rome.
Kwa wiki mbili zilizopita, maofisa mbalimbali wa Vatican wamekuwa wakifikiri kwamba Papa angeanza kuvaa mavazi meusi na kutumia jina la Askofu Mstaafu wa Rome ili kuepuka mkanganyiko na mrithi wake.
0 comments:
Post a Comment