RAIS Mwai Kibaki wa Kenya amehimitimisha ziara ya siku mbili nchini
Tanzania kwa kuwaaga wananchi wa taifa hilo huku akihimiza kuzidisha
ushirikiano wa ujirani mwema baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Rais Kibaki ambaye aliambatana na ujumbe wa maafisa kadhaa, ametumia ziara hio kutoa shukurani kwa wananchi wa Tanzania ambao amewalezea kama marafiki wema kwa Kenya na amehaidi kuendelea kushirikiana nao hata atapoondoka madarakani baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika March 4.
Kwa heri Afrika Mashariki
Rais Kibaki ametumia jukwaa la Tanzania kutoa salamu za, kwa heri kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kile kinachoelezwa kuwa kama moja ya agenda yake ya kutambua diplomasia yaTanzania ambayo ilifanikisha kumaliza mzozo uliozuka baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007.
Tamko kuhusu uchaguzi wa Kenya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania.
Rais Kikwete hata hivyo ametaka kufanyika kwa uchaguzi wa haki na huru ili kuepuka hali yoyote ya sintofahamu.
Kwa upande wake rais Kibaki amasema kuwa yuko tayari kukabidhi madaraka kwa mgombea yoyote atayeshinda katika uchaguzi huo ambao unatupia macho na Jumuiya za kimataifa.
Kuhusu uimarishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Mwai Kibaki alizitaka nchi wanachama kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa madai kuwa ndiyo lugha mama inayoweza kuwaunganisha wananchi wa eneo hili.
http://www.dw.de
0 comments:
Post a Comment