MKURUGENZI wa Upelelezi wa makosa ya Jinai, (DCI), Robert Manumba, aliyepelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi amepata nafuu kiasi cha kuanza kutembea na kufanya mazoezi ya viungo.
Akizungumza na Habarimpya.com hivi punde huku akiomba jina lake lisiandikwe mtandaoni mmoj wa watu wakaribu walioambatana na DCI Manumba alidai kwamba hali ya mgonjwa ni nzuri kwa sasa na amelazwa katika Hospitalini ya kijeshi ya mjini Pretoria aliyowahi kulazwa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela Desemba mwaka jana.
"Hali ya DCI kwa sasa ni nzuri, tofauti na tulivyotoka Tanzania, kwakweli hivi sasa anaendelea vizuri, wiki iliyopita alianza kujitambua na hivi sasa ameanza kufanya mazoezi ya viungo" kilisema chanzo hicho cha habari kutoka Afrika Kusini.
Kuhusu siku ya kurudi nchini chanzo hicho.
Alieleza kwamba, "Kwa sasa hatuwezi kurudi Tanzania kwa sababu madaktari wameshauri kwamba aendelee kuwa chini ya uangalizi wao kwa sababu bado kuna vipimo vinavyosubiriwa".
Kwa Upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso akizungumza na juu ya taarifa hiyo alisema kwamba hali ya DCI Manumba inaendelea vizuri kwani afya yake inazidi kuimarika kila wakati.
DCI Manumba alipelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi January 24
mwaka huu akiwa mahututi baada ya kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan.
Chanzo Habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment