Kwa ufupi
Simba wangeweza kwenda mbele mapema dakika ya nne
kama siyo Mrisho Ngasa kushindwa kumalizia kwenye kamba piga nikupige
kwenye lango la Prisons.Prisons walijibu shambulizi dakika ya 12 baada
ya shuti kali la Elias Maguli kupaa juu sintimeta chache kwenye lango la
Simba.
BAADA ya kukusanya pointi mbili katika michezo miwili, Mabingwa
wa Ligi Kuu Bara, Simba jana walipata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi
ya timu inayoshika nafasi ya 11 kwenye msimamo, Prisons ya Mbeya.
Wakati Simba wakijiimarisha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo, Azam FC iliendelea ‘kuwamwagia’ presha vinara Yanga kufuatia kuifunga JKT Ruvu mabao 4-0.
Yanga inaendelea kuongoza baada ya kujikusanyia pointi 33 sawa na Azam inayoshika nafasi ya pili, na Simba pointi 30 nafasi ya tatu.
Katika mchezo wa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, makocha wa pande zote mbili walilalamika, huku yule wa Simba, Patrick Liewig akilalamika ubovu wa kiwanja, na Kocha wa Prisons, Jumanne Charles akimtuhumu mwamuzi kuchezesha vibaya.
Kiungo Amri Kihemba ndiye aliyekuwa shujaa wa Simba baada ya kufunga bao hilo pekee kipindi cha kwanza.
Simba wangeweza kwenda mbele mapema dakika ya nne kama siyo Mrisho Ngasa kushindwa kumalizia kwenye kamba piga nikupige kwenye lango la Prisons.
Prisons walijibu shambulizi dakika ya 12 baada ya shuti kali la Elias Maguli kupaa juu sintimeta chache kwenye lango la Simba.
Elias alishindwa tena kuwanyanyua mashabiki wa Prisons baada ya kushindwa kuusukumizia nyavuni mpira kufuatia kipa wa Simba Juma Kaseja kutoka langoni.
Elias aliyekuwa akiisumbua ngome ya Simba muda mwingi wa mchezo, atajilaumu kwa kuwa kikwazo cha kuinyima mabao Prisons baada ya kupoteza nafasi nyingi.
Bao la Simba lilifungwa na Amri Kiemba baada ya kuunganisha wavuni pasi ya kiungo, Haruna ‘Boban’ Moshi katika dakika ya 36.
Mshambualiji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel anayeichezea Prisons, alichukizwa kwa kupumzishwa dakika ya 55 na kuingia Jeremiah Juma.
Katika kuonyesha kuchukizwa kupumzishwa, Gabriel alikataa kupokea chupa ya maji kutoka kwa daktari wa timu, Henry Andrew wakati akienda kwenye benchi.
Kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam walikuwa na sherehe ya kuhesabu mabao baada ya kuionea JKT Ruvu kwa kuitandika mabao 3-1 katika mchezo mwingine wa ligi.
Ushindi huo umewafikisha pointi 33, sawa na vinara Yanga ambao hawakuwa na ratiba ya mechi za katikati ya wiki, lakini wanaendelea kubaki kileleni.
Sherehe hiyo mjini Mbagala, ilianza dakika ya pili baada ya Wazir Salum kufunga bao la kuongoza akimalizia pasi ya Himid Mao.
Mshambuliaji John Bocco aliipatia Azam bao la pili kwa shuti kali dakika moja kabla ya filimbi ya mapumziko kufuatia gonga safi na Humphrey Mieno.
Ruvu waliorudi dimbani kipindi cha pili wakitarajia kurejesha mabao mawili waliyofungwa, walishitukia wakifungwa bao la tatu.
Bao hilo lilipachikwa wavuni na mshambuliaji Hamis Mcha katika dakika ya 46, aliyemalizia wavuni mpira kwa shuti kali kutokana na mpira wa krosi ya Himid.
Abdi Kassim aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Bocco, alitumia dakika mbili tu uwanjani kufunga bao la nne baada ya kuvunja mtego wa kuotea na kuingia ndani ya 18 na kufunga kwa shuti kali dakika ya 74.
0 comments:
Post a Comment