Mchinjaji akionyesha nyama halali kutoka machinjioni
kwenye maeneo ya Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam. [Deodatus Balile/Sabahi.
Na Deodatus Balile, Dar es Salaam
WAKRISTO wa Tanzania wamezuiliwa kwa muda kuchinja wanayama kwa ajili ya matumizi hadi serikali iteue kamati baina ya dini kutafuta ufumbuzi wa suala hili la uchinjaji kati ya Waislamu na Wakristo.
Agizo hilo limetolewa baada ya miezi zaidi ya
mitatu ya wasiwasi na mapigano katika mikoa ya Geita na Mwanza kuhusu uchinjaji
wa wanyama.
"Kwa kawaida Waislamu (ndio ambao
huchinja wanyama) katika nchi hii, lakini tuna mzozo huu na nimeunda kamati ya
viongozi wa dini kutafuta suluhisho la kudumu," Waziri Mkuu Mizengo Pinda
aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi (tarehe 16 Februari) baada ya mkutano
na viongozi wa Kiislamu na Kikristo katika mkoa wa Mwanza.
"Kwa hiyo, (wakati)kamati hii itakapokuwa ikifanya kazi kwa juhudi kupata suluhisho la kudumu,
Waislamu wataendelea kufanya kazi hii kwa ajili yetu sisi sote."
Kutoafikiana kulifikia kilele huko Buseresere
tarehe 11 Februari wakati vijana wa Kiislamu walipopambana na kikundi cha
Wakristo ambao walichinja ng'ombe na mbuzi wawili kwa ajili ya kuuza katika
soko la ndani.
Mapambano hayo yalisababisha mchungaji
Mathayo Machila kukatwa kichwa, na kujeruhi wengine kadhaa na mali muhimu
kuharibiwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita Paul
Kasabago alisema watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio, akiwemo Mchungaji
Pastor Isaya Rutta, ambaye alichinja mifugo katika viwanja vya kanisa.
Watu
wengine wawili wanaoshikiliwa ni wa upande wa kanisa la Rutta. Kasabago alisema
watashitakiwa kwa kukiuka sheria za afya, wakiwachochea wananchi na kusababisha
kifo cha Machila.
Polisi bado haijamkamata yeyote anayetuhumiwa
kufanya vurugu dhidi ya Machila.
"Sheria inasema kwamba mnyama yeyote
anayechinjwa aidhinishwe na mganga wa mifugo mwenye sifa (ili kuhakikisha)
anafaa kuliwa na binadamu," Kasabago aliiambia Sabahi.
"Kinyume na
hivyo, unahatarisha afya za walaji."
Rais
Jakaya Kikwete alilaani vurugu, akisema vita vya kidini sio maslahi mazuri
ya Tanzania. "Tumeishi kwa zaidi ya miaka 50 bila ya kuwa na ugomvi
unaohusiana na imani zetu kama Waislamu na Wakristo," alisema huko Dodoma.
"Ni ujinga kugombana kwa ajili ya haki
ya kuchinja," alisema.
Kikwete alimtuma Waziri wa Mambo ya Ndani
Emmanuel Nchimbi huko Buseresere kusuluhisha jamii zenye mgogoro kuhusu haki ya
kuchinja wanyama.
Nchimbi aliiambia Sabahi kwamba hali sasa
imedhibitiwa, kwa kuwa mazungumzo yanaelekea katika "mwelekeo mzuri".
Aliomba kwamba wale wanaohusika na vurugu watakabiliwa na adhabu za kisheria.
Utoaji kazi za machinjioni waibua maswali ya kidini
Nchini Tanzania machinjio yanamilikiwa na halmashauri za miji. Kwa miaka 50, ilikuwa ni desturi kwa machinjio kuwa na wafanyakazi wa Kiislamu, kufuatia miongozo ya Kiislamu.
Hatimaye nyama huuzwa
katika mabucha kwa ajili ya uuzaji wa rejereja.
Juvenary Mwaikambo, mwenye umri wa miaka 46,
ambaye huuza nguruwe katika Banana Bar huko Dar es Salaam, alisema anajua
machinjio mawili maalumu ya nguruwe ambayo Waislamu hawatachinja, lakini watu
wachache sana wanayatumia.
"Ninajua ni kinyume cha sheria kuchinja
nguruwe nyumbani, lakini ni ghali sana kuchinjia machinjioni," Mwaikambo
aliiambia Sabahi.
"Wanatoza shilingi 5,000 (Dola 3.10) kwa ajili ya
kuchinja na mganga wa mifugo anapaswa kuidhinisha nyama kwa kuigonga muhuri.
Kama [mganga wa mifugo] asema haifai kwa matumizi ya binadamu, inatakiwa
kufukiwa … kuna kero nyingi katika machinjio."
Aran Mashimba, mwenye umri wa miaka 48, mkazi
wa Buseresere, alisema suluhisho la mgogoro huo ni kuwa na machinjio tofauti
kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa imani zote.
"Sio tu kwa ajili ya kuwaridhisha
waumini wa Kiislamu, ni zaidi ya hilo," Mashimba aliiambia Sabahi.
"Uchinjaji wa nyama ni tasnia kubwa ambayo inazalisha ajira. Kufanyika na
Waislamu tu ni kutunyima (Wakristo) fursa za ajira."
Sheikh Suleiman Mtindi wa Mwanza, ambaye
alishiriki katika mkutano wa pamoja uliofanyika Jumapili pamoja na Pinda, pia
alipendekeza kutenganisha machinjio.
Pinda alilikataa wazo hilo, hata hivyo,
alisema litasababisha mgawanyo mkubwa.
CHANZO http://sabahionline.com
0 comments:
Post a Comment