Kwa ufupi:
Katika mchezo huo uliozikutanisha timu mbili katika
nafasi ya kwanza na pili kwenye msimamo, ulishuhudia mwamuzi Hashim
Abdallah akitolewa uwanjani chini ya ulinzi wa polisi.
Kiungo wa Yanga, Simon Msuva (kulia) akijaribu kutafuta njia ya kumtoka
kiungo wa Azam, Kipre Balou wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Bara kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda bao 1-0. Picha na
Michael Matemanga.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
Mshambuliaji
wa Yanga Jerry Tegete (kuli) akijaribu kumchambua kipa wa Azam Fc,
Mwadin Ally, wakati wa mchezo huo, ambapo Tegete alikosa baada ya kipa
huyo kuudaka mpira huo.
WATANI
WA JADI BWANA!!!!, Mashabiki wa Yanga, wakiwakebehi watani wao
Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Azam Fc, kwa Bango lenye
Ujumbe huu. ''Msomaji soma mwenyewe''.
Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga, waliojitokeza kuishangilia timu yao leo, ambao wanakadiliwa kuwa kama 25,0000 hivi.
Kikosi
cha Azam Fc kilichoanza.
Beki
wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akimkabili mshambuliaji wa Azam,
Kipre Tchetche, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Niyonzima baada ya kutupia bao.(PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)
VINARA wa msimamo, Yanga jana walipiga hatua muhimu kuelekea kulinasa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kutumia jasho jingi kupata ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Azam, shukrani kwa bao pekee kupitia kwa Haruna Niyonzima.
Katika mchezo huo uliozikutanisha timu mbili
katika nafasi ya kwanza na pili kwenye msimamo, ulishuhudia mwamuzi
Hashim Abdallah akitolewa uwanjani chini ya ulinzi wa polisi.
Hali hiyo ilitokea mara baada ya filimbi ya mwisho
kupulizwa kwa wachezaji wa Azam kumvamia kwa lengo la kutaka kumpiga
kwa madai ya kuibeba Yanga.
Matokeo hayo yalikuwa kicheko kikubwa kwa Kocha wa
Yanga, Ernest Brands aliyesema, kikosi chake kilistahili ushindi, na
kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuelekea kutwaa taji.
Ushindi huo wa Yanga umehitimisha uonevu wao mbele
ya Azam, kwani imeifunga mechi zote mbili msimu huu na kuvuna pointi
sita. Mzunguko wa kwanza walishinda 2-0.
Ushindi huo pia umekoleza kasi ya mbio za ubingwa,
kwani pamoja na kuwa nyuma kwa mchezo mmoja dhidi ya Azam, bado
inaendelea kuongoza baada ya kufikisha pointi 39.
Azam inabaki nafasi ya pili ikiwa na pointi zake
33, na mabingwa watetezi, Simba wanaoshuka dimbani leo wanashika nafasi
ya tatu ikiwa na pointi 31.
Iliwachukua Yanga dakika moja baada ya filimbi ya kuanza mchezo kupulizwa kulifikia lango la Azam kwa shambulizi kali.
Jerry Tegete akiwa kwenye nafasi nzuri alipiga
kichwa dhaifu kilichodakwa na Mwadin Ally kufuatia kazi nzuri
iliyofanywa na Saimon Msuva.
Dakika ya tano, Hamis Kiiza nusura aipatie bao
Yanga kama siyo shuti lake kali kudakwa na Mwadini, huku Azam nao
wakijibu shambulizi dakika moja baadaye Humphrey Mieno kupiga shuti kali
lililokwenda nje ya lango.
Kipre Tchetche naye alikaribia kufunga dakika ya 9
kama siyo shuti lake kali kukosa shabaha lango la Yanga na kwenda nje
dakika ya tisa.
Yanga iliyocheza kwa kuonana vizuri sehemu ya
kiungo, ilishindwa kufanya matokeo kuwa 1-0 dakika ya 16 baada ya Tegete
kupiga shuti ‘cha mtoto’ na kudakwa na Mwadin.
0 comments:
Post a Comment