NI KIWANDA KINACHOTENGEZA FULANA ZA MICHEZO AINA MBALIMBALI.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza nguo cha Mazava kilichopo Msamvu Manispaa ya Morogoro wakiwa katika picha tofauti wakati wakipatiwa huduma ya kwanza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kutokea hitilafu ya umeme na kusababisha wafanyakazi zaidi 60 kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana baada ya kukanyaganya.
Picha JumaMtanda.Blogspot.com
Akizungumza na Mwandishi wa Blog ya JumaMtanda.Blog.com katika hospitali ya mmoja wa majeruhi aliyenusurika katika tukio hilo Mrisho Kaguna wodi namba moja alisema kuwa walipatwa na mkasa huo jana saa 3:45 asubuhi wakati wakiwa katika shughuli za uzalishaji mali kiwandani hapo.
Kaguna alisema kuwa baada ya kupatwa na tatizo hilo walipatiwa matibabu kwenye zanahati ya kiwanda hicho kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Wafanyakazi Waliolazwa ni Amina Hamad, Elizabeth Gasper, Nesteria Erick, Rosa Mohamed, Upendo Makamba, fatuma Saidi, Mwanahamisi Seleiman, Mary Juma, Asha Maysa, Rotiwa Abert, Prisca Mlau, Rotiwa Abert, Joyce Mtonga, Albertina John, Getrude Bakari, Asha Saidi mwanamkombo Almas na Halima Kalwa.
Wengine ni Afrazia Shadrack, Nasra, Fide, Higa Zakaya, Gemi Issa, Agnes Adam, Tulia Nasasu, wasiojulikana wawili, Aneth Mesa, Salma Samuel, Salma Samwel, na ambao wamelazwa wodi namba nane huku wengine wakilazwa wodi namba tatu.
Naye majeruhi, Getrude Bakari aliyelazwa wodi namba tatu alisema kulisika kishindo kikubwa na ghafla hewa nzito na kuanza kukimbilia nje ya kiwanda lakini walijikuta wakikanyagana vibaya.
Akizungumzia majeruhi hao, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Ritha Lyamuya alisema kuwa majira ya saa sita hadi saa 7 mchana walipokea majeruhi zaidi ya 70 ambao wengi wao ni wanawake ni 65 na wanaume wawili.
Alisema hali zao mpaka jana jioni zilikuwa zinaendelea vizuri na wengine walipatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa.
0 comments:
Post a Comment