Chanzohttp://www.habarimpya.com.
WAKATI kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu,
Sheikh Ponda Issa Ponda, ikiendelea katika Mahakama ya hakimu Mkazi
Kisutu wafuasi wake 52 kati ya 53 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya
maandamano haramu wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.
Hata hivyo mahakama hiyo ilimwachia huru mshtakiwa mmoja, Waziri Omar
Toy, ambaye alikuwa mshtakiwa wa 48 katika kesi hiyo baada ya kuridhika kuwa hana hatia kutokana upande wa mshtaka kushindwa kuthitibisha mashtaka dhidi yake.
Wafuasi hao wa Ponda walihukumiwa adhabu hiyo jana na Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikiana na hatia katika makosa
matatu yaliyokuwa yakiwakabili kati ya manne.
Wafuasi hao wa Ponda walikamatwa Februari 15 wakidaiwa kufanya
maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa lengo la
kumshinikiza aondoe zuio la dhamana dhidi ya Ponda na mwenzake, Mukadamu Swalehe, wanaokabiliwa na kesi ya uvamizi wa kiwanja cha Chang’ombe Markazi.

Akisoma
hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alisema kuwa baada ya
kusikiliza ushahidi na hoja za pande zote pamoja na
vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ameridhika, kuwa upande wa
mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka matatu dhidi ya washtakiwa hao.
“Katika kosa la kwanza ninawahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela,
na kosa la pili pia mwaka mmoja jela na tatu mwaka mmoja jela. Adhabu
zote zinakwenda kwa pamoja.”alisema Hakimu Fimbo.
Aliyataja mashtaka hayo ambayo
washtakiwa walipatikana na hatia kuwa ni shtaka la kwanza la kula njama
za kutenda makosa, la pili, kufanya maandamano yaliyozuiwa na Jeshi la Polisi na la tatu kufanya mikusanyiko haramu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Hata hivyo Hakimu Fimbo alisema kuwa katika shtaka la nne
la uchochezi wa kutenda kosa lililokuwa likiwakabili washtakiwa wanne,
upande wa mashtaka umeshinda kulithibitisha.
“Mahakama imeridhika na ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashtaka
kuwa umethibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa
wa 48.”, alisema Hakimu Fimbo na kuongeza:
“Hivyo mahakama imewatia
hatiani washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48, katika shtaka la
kwanza, la pili na la tatu, na katika shtaka la nne, mahakama imeona
kuwa washtakiwa hawana hatia.”
0 comments:
Post a Comment