SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage kupinduliwa na wanachama wa klabu hiyo, uongozi wa mwenyekiti huyo umewasilisha barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga mapinduzi hayo.
Kwa muujibu wa taarifa kutoka TFF zinadai kwamba Uongozi wa Simba imeandika barua hiyo ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa Simba.
Katika kikao hicho kilichofanyika jana katika ukumbi wa Starlight, jijini Dar es Salaam Rage ambaye yuko nchini India kwa matibabu alipinduliwa na kundi la wanachama 698.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.
Chanzo http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment