Kwa ufupi
Koplo Nko alipatwa na mauti hayo juzi saa 7:00
mchana eneo la Bamaga, baada ya msafara wa Rais Kikwete kupita, Baada ya
msafara huo kupita eneo hilo, Koplo Nko aliamua kuingia barabarani
kuongoza magari, punde gari aina ya Land Rover.
RAIS JAKAYA KIKWETE.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiwasiliana kwa simu baada ya
gari linalodaiwa kumgonga polisi wa kikosi hicho wakati akiongoza
msafara wa Rais Jakaya Kikwete juzi eneo la Bamaga Mwenge, kukwama eneo
la Tabata relini. Gari hilo lilikamatwa jana Dar es Salaam. Picha na
Fidelis Felix.
Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete jana aliwaongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa Polisi wa Kikosi cha Barabarani, Koplo Elikiza Nko aliyefariki kwa kugongwa na gari iliyovamia msafara wa Rais.
Wakati Rais Kikwete akishiriki tukio hilo, polisi inawashikilia watu wawili kwa mahojiano kuhusuiana na tukio hilo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed
Mpinga alisema watu hao wanahojiwa wapo mikoa tofauti; Dar es Salaam
na Arusha.
Mpinga alisema lengo la kuwashikilia watu hao, ni
kutaka kuhakikisha wanampata mhusika halisi wa tukio hilo na hatimaye
kumfikisha mahakamani.
Koplo Nko anatarajiwa kuzikwa Machi 21, mwaka huu kwenye makaburi ya Bunju A, Manispaa ya Kinondoni.
Jana, Rais Kikwete na viongozi wengine wa Serikali walikwenda kwenda nyumbani kwa marehemu Nko kufariji ndugu wa askari huyo.
Koplo Nko alipatwa na mauti hayo juzi saa 7:00
mchana eneo la Bamaga, baada ya msafara wa Rais Kikwete kupita.
Baada ya msafara huo kupita eneo hilo, Koplo Nko aliamua kuingia barabarani kuongoza magari, punde gari aina ya Land Rover ambalo ni mali ya Kanisa la Tanganyika Assemblies of God (TAG) lilichomoka kusikojulikana na kumgonga askari huyo.
Rais Kikwete ambaye akiendelea na ziara yake ya siku mbili.
Baada ya msafara huo kupita eneo hilo, Koplo Nko aliamua kuingia barabarani kuongoza magari, punde gari aina ya Land Rover ambalo ni mali ya Kanisa la Tanganyika Assemblies of God (TAG) lilichomoka kusikojulikana na kumgonga askari huyo.
Rais Kikwete ambaye akiendelea na ziara yake ya siku mbili.
Awali, akiwa viwanja vya Mnazi Mmoja alisisitiza itolewe adhabu kali kwa wauguzi wanaobainika kughushi vyeti vya taaluma.
Alitoa kauli kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka
60 tangu kuundwa kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania, hadi sasa
baraza hilo limefanikiwa kuwakamata wauguzi watano waliokutwa na makosa
hayo. “Hawa ni watu wa ajabu sana, kama tatizo litakuwa ni sheria basi
iongezewe makali,” alisema Rais Kikwete.
0 comments:
Post a Comment