BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIFO CHA RAIS CHAVEZ, MAJONZI, SIMANZI VYATALA CARACAS NCHINI VENEZUELA.

Kwa ufupi
Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro alikuwa  kiongozi wa shughuli nzima ya kuuaga mwili wa Chavez.
 Jeneza lenye mwili wa Rais wa Venezuela Hugo Chevez. 
 
SIMANZI na majonzi vilitawala wakati  raia wa Venezuela walipokuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa rais wa nchi hiyo, Hugo Rafael Chavez.

Mwili wa marehemu Chavez ulilazwa katika Kituo cha Mafunzo ya Jeshi katika Mji Mkuu wa Caracas  mapema asubuhi ya jana na  ulipitishwa mbele ya umati wa wafuasi wake tayari kwa kuzikwa .

Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro alikuwa  kiongozi wa shughuli nzima ya kuuaga mwili wa Chavez.

Mamia ya waombolezaji walionekana wakiangua vilio, baadhi walibeba picha za kiongozi huyo na wengine wakitamka Maneno ya kumuenzi, kumsifu na kuonyesha  pengo walilo nalo sasa yalisikika.

Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo shupavu .


Chavez alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 baada ya kuugua saratani kwa zaidi ya miaka miwili.

Jeneza lake lililokuwa limefunikwa bendera ya nchi hiyo liliwekwa katika ukumbi wa kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini

Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwamo maofisa wa Serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini, kama Rais wa Bolivia, Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner,
 ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa Chavez.

Maduro alitangaza kuwa uchaguzi mwingine wa kumpata mrithi wa Chavez utafanyika ndani ya siku 30  baada ya mazishi ya Chavez.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: