Kwa ufupi
Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini na
kuthibitishwa na uongozi wa Tef zinasema madaktari wanaomtibu Kibanda
walibaini madhara zaidi ambayo ni pamoja na kukatika kwa mfupa laini
(fizi) unaounganisha pua na mdomo pamoja na kulegea kwa meno takriban
sita.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alitekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya na juzi alasiri alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na uongozi wa Tef zinasema madaktari wanaomtibu Kibanda walibaini madhara zaidi ambayo ni pamoja na kukatika kwa mfupa laini (fizi) unaounganisha pua na mdomo pamoja na kulegea kwa meno takriban sita.
Taarifa ya Tef iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Neville Meena imesema athari hiyo imesababishwa na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumng’oa meno...“Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake.”
Kibanda alitekwa na watu wasiofahamika ambao walimshambulia kwa nondo na mapanga na kumng’oa meno mawili, kucha na kumjeruhi jicho la kushoto usiku wa kuamkia juzi.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz
Madaktari katika Hospitali ya Millpark, Afrika Kusini wamebaini
madhara zaidi aliyopata Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef),
Absalom Kibanda kutokana na unyama aliofanyiwa na watu wasiojulikana
usiku wa kuamkia juzi.
Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alitekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya na juzi alasiri alisafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na uongozi wa Tef zinasema madaktari wanaomtibu Kibanda walibaini madhara zaidi ambayo ni pamoja na kukatika kwa mfupa laini (fizi) unaounganisha pua na mdomo pamoja na kulegea kwa meno takriban sita.
Taarifa ya Tef iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Neville Meena imesema athari hiyo imesababishwa na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji kumng’oa meno...“Kutokana na hali hiyo ana maumivu makali sana kwenye kinywa chake.”
Kuhusu meno, Meena alisema hayo sita yaliyoelezwa kwamba yamelegea ni mbali na yale mawili yaliyong’olewa katika tukio la awali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Tef, Kibanda
alifanyiwa uchunguzi wa kitabibu na baadaye jana jioni, madaktari
walikuwa wakitarajiwa kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili
kutafsiri maana ya matokeo yake kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata
au aina ya tiba inayopaswa kutolewa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006),
Hussein Bashe alisema madaktari walianza kazi hiyo baada ya Kibanda
kufikishwa hospitali hapo juzi usiku.
"Tunashukuru walifika salama, tatizo lilikuwa Uwanja wa Ndege wa Johannesburg, walichelewa kama saa moja hivi kwa masuala ya Uhamiaji, lakini baada ya hapo alipelekwa hospitali.”
"Tunashukuru walifika salama, tatizo lilikuwa Uwanja wa Ndege wa Johannesburg, walichelewa kama saa moja hivi kwa masuala ya Uhamiaji, lakini baada ya hapo alipelekwa hospitali.”
“Kwa kuwa alipigwa sindano ya kutuliza maumivu
pamoja na usingizi wakati anaondoka, sasa baada ya kuimarika kiakili,
alipelekwa chumba cha upasuaji kuangalia jinsi gani ya kulihudumia jicho
na hicho kilikuwa kitu cha kwanza na wakati huohuo alianza kufanyiwa
uchunguzi ili kujua ameumizwa kiasi gani.”
Katika hatua nyingine, uongozi wa Taasisi
iitwayo Southern African Investigative Journalism Forum, jana
ulimtembelea Kibanda hospitalini na kueleza masikitiko yake kuhusu
yaliyomkuta.
Uongozi huo uliahidi kushirikiana na taasisi
za kihabari za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata
majawabu ya nini kilichojiri na sababu zake.
Leo Tef watakuwa na mkutano wa wahariri wote kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza kuhusu matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari kikazi.
Leo Tef watakuwa na mkutano wa wahariri wote kujadili hatua zaidi za kuchukua kwa maana mbili; kwanza kuhusu matibabu na afya ya Kibanda na pili usalama wa waandishi wa habari kikazi.
Kibanda alitekwa na watu wasiofahamika ambao walimshambulia kwa nondo na mapanga na kumng’oa meno mawili, kucha na kumjeruhi jicho la kushoto usiku wa kuamkia juzi.
0 comments:
Post a Comment