BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MASHINDANO YA VYUO VYA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA YAANZA KUTIMUA VUMBI MOROGORO.


Mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi akipiga mpira na kufunga bao la penalti ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa mashindano ya vyuo vya Utumishi wa umma Tanzania katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
DC Amanzi akizungumza na wanamichezo muda mfupi kabla ya mashindano hayo kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya Jamhuri Morogoro.
Mchezaji wa Tabora Sport Club Maria Musiba kulia akitafuta mbinu ya kufunga huku mchezaji mwenzake Grace Allan akijiandaa kutoa msaada dhidi ya wachezaji wa timu ya Magogoni Dar es Salaam, Georgia Lugalinda na Matrida Swai wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya vyuo vya utumishi wa umma Tanzania katika uwanja wa jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo Tabora ilishinda kwa vikapu 35-5 katika uwanja wa ndani Jamhuri mkoani Morogoro.
KIKOSI CHA TIMU YA TABORA KILICHOIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 DHIDI YA MAGOGONI DAR ES SALAAM
KIKOSI CHA TIMU YA MAGOGONI DAR ES SALAAM KILICHOPOKEA KIPIGO KUTOKA KWA TABORA KWA USHINDI WA BAO 1-0.
Mchezaji wa timu ya Singida akijaribu kuwatoka wachezaji wa Magogoni Dar es Salaam katika mchezo wa basketiboli ambapo Singida ilipoteza kwa vikapu 44-28. 
PICHA NA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya sport Club ya chuo cha utumishi wa umma Tanzania tawi la Mtwara imeanza vema mashindano ya vyuo vya utumishi Tanzania baada ya timu zake kufanya vizuri katika michezo ya ufunguzi yalioanza kutimua vumbi katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Nyota njema kwa chuo hicho ilianza kwa kushinda michezo mitatu huku katika mchezo wa soka ikiambulia kichapo katika michezo hiyo ya ufunguzi wa mashindano hayo.

Ni mchezo wa netiboli iliyoanza kupeleka furaha baada ya kuilaza Singida kwa vikapu 40-9 kabla ya vijana wa basketibal kuinyuka Tabora kwa 58-32 wakati timu ya wavu nayo ikifanikiwa kupata ushindi wa seti 3 kwa 2 dhidi ya Singida huku katika mchezo wa soka ikiambulia kutandikwa bao 2-0 na Tabora.

Katika michezo mingine chuo cha Magogoni Dar es Salaam kilipokea kichapo cha kufungwa bao 1-0 na Singida kwa upande wa mchezo wa soka, Magogoni ilipata ushindi katika mchezo wa baskatiboli kwa vikapu 44-28 dhidi ya Singida kabla ya kupoteza ushindi mungine katika mchezo wa wavu ka seti 2-3 na Tabora.

Michezo ya mashindano hayo yanaendelea katika uwanja huo wa jamhuri Morogoro kwa michezo ya soka, basketiboli, wavu, netiboli ambayo hufanyika asubuhi na jioni ikishirikisha vyuo vya Mtwara, Tabora, Singida na Magogoni Dar es Salaam ambayo yatafikia tamati marchi 27 mwaka huu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: