MSHINDI wa urais nchini Kenya anatarajiwa kutangazwa mapema leo, baada
ya kukamilika kwa zoezi la kuhakiki matokeo ya mwisho, ambapo Uhuru
Kenyatta anaongoza kwa kuwa na asilimia 50.03.
Kuchelewa huko kulitokana na hitilafu iliyosababishwa na kukwama kwa mfumo wa elektroniki wa kujumlisha kura na kuwasilisha matokeo kupitia runinga.
Shughuli ya kujumlisha kura ilikamilika saa nane usiku na wawakilishi wa wagombea urais walianza zoezi la kuthibitisha hesabu hizo.
Kura hiyo ambayo matokeo yake yalisubiriwa kwa kwa hamu imehusisha wagombea wanane ambao ni Waziri Mkuu Raila Odinga Manaibu wake wawili Uhuru Kenyatta na Musalia Mudavadi, James Ole Kitiapi Peter Keneth, Martha Karua, Mohammed Abduba Diba na Wakili Paul Muite.
Kura ya hasira dhidi ya ICC?
Dr. David Matsanga, mtaalamu wa usuuhishi wa migogoro, ameulezea ushindi wa Kenyatta kama kura ya hasira dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC iliyowafungulia mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinaadamu, Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.
Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto, ambao wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya ICC.
Hapo jana kundi moja linalojiita 'African Centre for Governance' lilienda mahakamani kutaka zoez zima la kujumlisha kura lisitishwe kwa madai kwamba shughuli ya uchaguzi ilikumbwa na udanganyifu na kutokana na kukwama kwa mfumo wa elektroniki wa kuhesabu kura.
Hata hivyo Jaji David Majanja wa Mahakama kuu alitupilia mbali ombo hilo na kusema hiyo ni kazi ya mahakama ya juu yaani Supreme Court.
Kwa mujibu wa katiba Rais Mpya atakayetangazwa hivi leo ataaapishwa siku kumi na nne zijazo.
0 comments:
Post a Comment