Arusha.Polisi
Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara(Chadema
),Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi
ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka
mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo
kabla ya kufikishwa mahakamana.
Mbunge
Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata
taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani kwani
wanapajua.
Hata
hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye mkutano
wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa kijiji,
kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike
Basotu viongozi wa wilaya.
Wananchi
365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo
pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo
hadi muafaka utakapopatikana.
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment