Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda
mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari
18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali
ya kijeshi kuendelea kupokea matibau.
Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu
ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa
juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya
ya rais wao.
Bwana Chavez amekua uongozini nchini
Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi
kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.
Ujumbe wa Jeshi.
Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa
wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama.
Pia jeshi limeahidi
kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito
kwa raia kuwa watulivu.
Chavez
- wasifu
Hugo Chavez alijitosa katika siasa za
Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika jeshi.
Aliongoza mapinduzi
dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa
kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka
hayo.
Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini baada ya ushindi
mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo.
Katika kuapishwa kwake mnamo
February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba mipango yake ya mabadiliko ya
kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu.
Alitimiza ahadi yake na kuiongoza nchi hiyo
katika mabadiliko ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa.
Alibadili muundo wa bunge na kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda
katiba mpya baada ya kura ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha rasilmali
ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta.
Sera kama hizi zilimfanya azozane na kampuni
za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa wa watu maskini.
Chavez
na jamii ya kimtaifa
Kutokana na urafiki wake na viongozi wa
mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro, ambaye walikuwa na
uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na Marekani, ambayo ni mshirika wake
mkuu wa kibiashara.
Chavez alipendwa nyumbani na wafuasi
wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini humo na katika nchi za nje.
Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini lakini pia kama muingiliaji wa
siasa za nchi jirani.
Katika miaka ya hivi karibuni alilenga kukabiliana na
masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu, kuinua uchumi wa nchi na
kukabiliana na rushwa.
0 comments:
Post a Comment