Kwa ufupi
Kwa matokeo hayo, Azam sasa imejihakikishia kucheza
Kombe la Shirikisho mwakani baada ya kufikisha pointi 48, ambazo
haziwezi kufikiwa na timu nyingine.http://www.mwananchi.co.tzMchezaji wa Coastal Union akikabiliana na miamba ya Azam FC.
TANGA.
KLABU ya Azam FC imeikabidhi rasmi ubingwa Yanga baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Coastal Union jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
KLABU ya Azam FC imeikabidhi rasmi ubingwa Yanga baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Coastal Union jana kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Nahodha Aggrey Morris akicheza mechi yake ya
kwanza tangu Takukuru ilipomsafisha katika kashfa ya kupokea rushwa,
aliifungia Azam bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya
59, lakini Danny Lyanga aliyeingia akitokea benchi aliwasawazishia
wenyeji katika dakika ya 72.
Kwa matokeo hayo, Azam sasa imejihakikishia
kucheza Kombe la Shirikisho mwakani baada ya kufikisha pointi 48, ambazo
haziwezi kufikiwa na timu nyingine, huku wakitoa nafasi kwa Yanga
kutwaa ubingwa wake wa 23 wa Ligi Kuu msimu huu wakiwa na pointi zake 56
ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote.
Katika mchezo huo, Kocha wa Azam, Stewart Hall
aliwaanzisha kwa mara ya kwanza, nahodha Morris na Erasto Nyoni
waliomaliza vifungo vyao, huku akiwa wamewapumzisha nyota wake kadhaa wa
kikosi cha kwanza.
“Tuliwapumzisha wachezaji wetu kadhaa ili
kujiandaa na mechi yetu ya Morocco kwa sababu ni ngumu na iliyojaa
ushindani.
Kwa jumla timu yangu ilicheza vizuri na nimevutiwa na jinsi Nyoni alivyocheza kwa kiwango cha juu,” alisema Hall.
Kwa jumla timu yangu ilicheza vizuri na nimevutiwa na jinsi Nyoni alivyocheza kwa kiwango cha juu,” alisema Hall.
“Tusingeweza kuizuia Yanga kutwaa ubingwa, kwa
sababu ni timu bora inayofundishwa na kocha bora, kwa namna yoyote
katika mechi tatu zilizobaki wasingekosa pointi moja.”
Wenyeji Coastal Union walianza vizuri na
kufanikiwa kufika katika goli kwa Azam katika dakika kwanza, lakini
shuti la Abdi Banda lilidakwa kwa ustadi mkubwa na kipa Mwadin Ally.
Azam walijibu mapigo dakika ya 13, baada ya shuti la Erasto Nyoni kupaa juu baada ya kazi nzuri ya Mwaipopo.
Mashabiki wa Coastal Union waliokuwa wamekaa
jukwaa la Old Tanga walijitahidi kushangilia kwa nguvu timu yao wakati
wa mapumziko walimfuta mwamuzi wakitaka kumpiga kwa madai kuwa
anapendelea Azam, lakini Polisi waliingilia kati.
Katika dakika ya 56, mshambuliaji Gaudence
Mwaikimba alichezewa vibaya na Razack Khalfan kwenye eneo la penalti na
mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani kutoa penalti iliyofungwa na nahodha
Morris.
Mshambuliaji Danny Lyanga aliyeingia akitokea
benchi kuchukua nafasi ya Selemani Selembe aliisawazishia Coastal Union
katika dakika ya 72.
0 comments:
Post a Comment