Kwa ufupi
Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu
wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na
askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo.
http://www.mwananchi.co.tzMbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa polisi siku za hivi karibuni.
http://www.mwananchi.co.tzMbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa polisi siku za hivi karibuni.
ARUSHA.
MAOFISA wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.
MAOFISA wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.
Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye
alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo.
Walifika nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini
walilazimika kusubiri hadi saa 9:10 walipomkamata Mbunge huyo baada ya
yeye mwenyewe kujisalimisha.
Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba “anaweza kuhatarisha amani”.
Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba “anaweza kuhatarisha amani”.
Mashuhuda waliokuwa karibu na anakoishi Lema, eneo
la Njiro Mwisho wa Lami, walisema polisi hao walifika wakiwa kwenye
magari manne na kwamba ili kuchunguza ndani ya uzio wa nyumba yake,
walipanda juu ya mabega ya wenzao huku wakielekeza mitutu ya bunduki
tayari kukabiliana na lolote ambalo lingejitokeza.
Baada ya kuchungulia baadhi yao walitumbukia ndani
ya uzio na kwenda kusimama mbele ya milango na madirisha ya nyumba ya
Lema na huku nyuma wengine walipanda tena kwenye mabega ya wenzao
kuendelea kuweka ulinzi kwa walioingia ndani.
Askari hao wanadaiwa kwamba waliwataka walinzi wa
nyumba hiyo iliyopo karibu na Chuo cha Ufundi Veta, kuwafungulia mlango,
lakini walinzi hao walikataa hivyo kuzua mabishano makali.
Kutokana na mabishano hayo, Lema aliyekuwa ndani
amelala alishtuka na kuanza kufuatilia na kubaini kuwapo kwa polisi nje
ya nyumba yake hiyo. Mke wa Lema, Neema alimpigia simu Katibu wa Wilaya
wa Chadema, Aman Golugwa kumwarifu kuhusu uwepo wa watu walioruka ukuta.
Golugwa jana alithibitisha kupokea simu ya mke wa
Lema na kwamba alipopata taarifa hizo alimwarifu Mkuu wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Arusha, Camillius Wambura ambaye
baadaye alimuahidi kwamba angefuatilia suala hilo.
“Baadaye alithibitisha kuwapo kwa polisi
waliotumwa kwa ajili ya kumkamata Lema lakini akasema amewapa maelekezo
ya kufuata taratibu za kawaida,”alisema Golugwa na kuongeza:“Baada ya
hapo, wale askari waliokuwa wameruka ukuta walitoka nje ya uzio”.
Habari zinasema wakati baadhi ya askari wanaruka
ukuta, wengine walibaki nje wakizingira uzio wa nyumba ya Lema huku
wakiwazuia viongozi wa Chadema waliokuwa eneo hilo kusogea.
Kukamatwa kwa Lema katika mtindo wa aina yake
kumefanywa saa chache tangu alipotoa kauli ya kukataa kujisalimisha
polisi, kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Mulongo aliagiza Lema akamatwe kwa tuhuma kwamba alichochea vurugu
katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walimzomea
Mulongo na kurushia mawe msafara wake wakati alipokwenda kusikiliza
malalamiko yao yaliyotokana na kuuawa kwa mwanafunzi mwenzao, Henry Kago
(22) ambaye alichomwa kisu na watu wasiofahamika wakati anatoka
kujisomea saa 4:00 usiku.
0 comments:
Post a Comment