BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BENKI YA CRDB YAKARABATI WODI HOSPITALI KWA GHALAMA YA SH 50 MIL MOROGORO.

 Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Daktari Seif Rashid utepe ikiwa ishara ya uzinduzi wa wodi ya watoto ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya benki CRDB kufanya ukarabati na kughalimu kiasi cha fedha sh50 Milioni mkoani Morogoro.
 Mandhali ya wodi ya watoto katika hospitali hiyo kama inayoonekana baadhi ya vitanda.


Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Daktari Seif Rashid (katikati) Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr Charles Kimei kulia na mkurunzi wa benki hiyo mkoa wa Morogoro, Pendo Assey wakati wakielekea kumsindikiza naibu waziri kuzidnua wodi hiyo ya watoto.
 Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii, Daktari Seif Suwed Rashid kulia akishirikiana na Mkurugenzi Mkuu benki ya CRDB, Daktari Charles Kimei kushoto kutundika chandarua kwenye kitanda katika wodi ya watoto.
 Wadau wa benki ya CRDB nao wakishiriki katika tukio la kutandika vitanda na kutundika chandarua katika vitanda vya wodi hiyo.
 Hapa ni kundi la wafanyakazi wa benki hiyo nao wakijumuika na watu wengine katika shughuli hiyo.
 Hapa Daktari Rashid akisoma hutuba mara baada ya kuzindua wodi hiyo iliyoambatana na upandaji wa miti ndani ya hospitali hiyo, kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr Charles Kimei kulia na kulia ni Mkurugenzi wa benki hiyo mkoa wa Morogoro, Pendo Assey.
 Mkurugenzi mkuu wa benki ya CRDB Dr Charles Kimei akizungumza jambo katika shughuli hiyo, kutoka kushoto ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo na kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi, Mkurugenzi wa benki hiyo mkoa wa Morogoro, Pendo Assey na naibu waziri Daktari Rashid.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi akizungumzaa jambo kwenye uzinduzi huo, kutoka kushoto ni Dr Charles Kimei, naibu waziri Daktari Rashid na Mkurugenzi wa benki ya mkoa wa Morogoro, Assey
 Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Godfrey Mtei kushoto akifurahia jambo na Dr Charles Kimei mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uzinduzi wa wodi hiyo.
 Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Rashid kushoto akisikiliza jambo kutoka kwa mmiliki wa mabasi ya Hood, Mohamed Hood mara baada ya hafla hiyo kumalizika.
 Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Rashid akiteta na Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro Dogfrey Mtei
 Sehemu ya viongozi mbalimbali wa hospitali hiyo, serikali na dini wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
 Hapa wageni waalikwa wakiwemo na wauguzi wa hospitali hiyo nao wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
 Picha ya pamoja viongozi wa serikali na wafanyakazi wa beki hiyo.

















Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: