BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI AKAMATWA KIJAJUSI.

 POLISI WATUMIA MBWA, MAOFISA USALAMA WA TAIFA, KUPANDISHWA KIZIMBANI JUMATATU IJAYO.
http://www.mtanzania.co.tz
HATIMAYE Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limetumia kila aina ya mbinu kutekeleza amri ya Mkuu wa Mkoa huo, Magesa Mulongo, kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Jeshi hilo, kwa kushirikiana na maofisa usalama wa taifa, askari wa upelelezi na askari wa kawaida, wakiwa na mbwa walivamia nyumbani kwa Lema saa 5 usiku kwa lengo la kumkamata, lakini walipata wakati mgumu kutoka kwa mlinzi wa nyumbani kwake hadi saa 9 usiku ndipo walipofanikiwa kuondoka naye.

Taarifa za askari kuvamia nyumbani kwa Lema, zilianza kusambaa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Arusha, juzi usiku saa 4 na kusababisha mamia ya wafuasi wa mbunge huyo kwenda eneo la Njiro kwa ajili ya kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea.


Habari kutoka eneo la tukio, zinasema kutokana na askari hao kufika usiku na kuwakuta walinzi wa Lema, waligoma kufungua geti na kusababisha malumbano.

Kutokana na kuibuka kwa malumbano hayo, Lema alilazimika kutoka ndani ili kujua chanzo cha malumbano hayo nje ya nyumba yake.

Akizungumzia tukio hilo, Lema alisisitiza kulishangaa Jeshi la Polisi na maofisa wengine wa usalama kwa kumvamia usiku wakati wana mawasiliano yake ya simu ya kiganjani.

“Nashangaa aina ya askari tulionao, wameshindwa kunipigia simu mpaka wananivamia usiku kama majambazi kuja kunikamata,” alisema Lema na kuongeza:

“Wamevamia na kuanza kutishia kupiga mabomu nyumba yangu, kama ningegoma kutoka nje na kujisalimisha,” alisema.

Hata hivyo, alisema baada ya kushauriana kwa kina na viongozi wake wa chama, aliamua mwenyewe kutoka nje na kujisalimisha mikononi mwa askari.

Kwa upande wake, mlinzi wa nyumbani kwa Lema, Calist Lazaro alidai alishindwa kuwafungulia askari hao kwa kuhofia usalama wa bosi wake.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kushikiliwa kwa Lema na kueleza mpaka jana, walikuwa hawajachukua maelezo yake.

Alisema Lema alifikishwa kituoni hapo juzi usiku na kuwekwa rumande ya wahalifu wa kawaida ili kusubiri taratibu za kutoa maelezo. 


Lakini taarifa tulizopata wakati tunakwenda mitamboni, zinasema Lema atafikishwa mahakamani Jumatatu ijayo.

“Bado hatutajua ni lini tutampeleka mahakamani kwa sababu ya vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu Arusha,” alisema Kamanda Sabas.

Lema amekamatwa kutokana na agizo la Mulongo, baada ya kudaiwa alichochea ghasia za wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, kufuatia kuuawa kwa mwenzao, Henry Kago (22), ambaye alikuwa mwaka wa pili.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: