Kwa ufupi
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.http://www.mwananchi.co.tzKamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani
MBEYA.
MSAIDIZAI wa zamani wa Padri (Katekisita) katika Kigango cha Kanisa Katoliki Kijiji cha Mkwajuni, Florian Mwamosi (70) amekufa baada ya kuzikwa akiwa hai katika kaburi moja na mtu anayedaiwa kumuua kwa njia ya kishirikina.
Tukio hilo limetokea katika Kitongoji cha Maweni kijijini hapo wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani
alikiri kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa lilitokea saa 9:00
mchana katika kij
iji hicho cha Maweni Mkwajuni wilayani Chunya.
iji hicho cha Maweni Mkwajuni wilayani Chunya.
“Marehemu aliuawa na wananchi wenye hasira kali
kwa kupigwa na mawe kwa tuhuma za kuhusika na uchawi na kusababisha kifo
cha Peter Robert,” alisema.
Kamanda Athumani alisema kuwa uchunguzi kuhusiana
na tukio hilo unaendelea na kwamba wahusika wote wa tukio hilo
wamekimbia na kuzihama nyumba zao, hivyo polisi wanaendelea na msako wa
kuwatia mbaroni watuhumiwa na kwamba tayari kaburi hilo limefukuliwa
jana kutenganisha maiti hizo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa marehemu
huyo ambaye alikuwa akituhumiwa kwa ushirikina aliwahi kuwa Katekista wa
kigango hicho hadi mwaka 2007.
Wameeleza kuwa Mwamosi alikwenda kuhudhuria
mazishi ya Peter Robert (28) katika kitongoji hicho cha Maweni, baada
ya kufuatwa nyumbani kwake na watu wakitaka aende kwa sababu yeye ni
mmoja wa wazee wa mila katika kitongoji hicho.
“Bwana Mwamosi alikuwa akituhumiwa kwa uchawi kwa
muda mrefu na wenzie wawili, hivyo alipofika makaburini ilianza
minong`ono ya watu na huku wengine wakiguna na ndipo alipoombwa aingie
kaburini kwa ajili ya kupokea jeneza lililobeba mwili wa marehemu Peter
Robert,” alisema mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina
moja la Joseph.
Alisema kuwa baada ya kuingia kaburini akiwa na
watu wengine watatu wenzake walitoka kwa haraka na kumwacha Mwamosi peke
yake ndipo kundi la watu waliokuwa eneo hilo la makaburi walianza
kumshambulia kwa kumpiga mawe huku wakimwamuru akae chini.
Shuhuda huyo alisema kuwa baada ya kukubali kukaa
chini akiwa ndani ya kaburi hilo, walianza kumfukia na alipofukiwa nusu
ya mwili wake waliingiza jeneza la marehemu Peter na kuliweka juu yake
na kuanza kulifukia kaburi hilo.
“Baada ya kukaa chini ndani ya kaburi hilo ndipo
walianza kumfukia kwa udongo na baadaye wakachukua jeneza la marehemu na
kuliweka juu yake, kisha kumfukia na udongo na taratibu za mazishi
ziliendelea kwa ajili ya marehemu Peter,”alisema.
Alidokeza kuwa chanzo cha tukio hilo ni marehemu
Robert kuugua ghafla tumbo, ndipo ndugu zake walipoamua kumpeleka kwa
mganga wa jadi kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya siku tatu
alifariki dunia.
0 comments:
Post a Comment