Kwa ufupi
Arusha: Kushikiliwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini
(Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa
upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.http://www.mwananchi.co.tz
ARUSHA:
KUSHKILIWA kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.
KUSHKILIWA kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kumeendelea kuibua sokomoko baina ya polisi kwa upande mmoja na wafuasi wa Chadema na familia yake kwa upande mwingine.
Arusha. Lema aliyekamatwa usiku wa manane kuamkia
Ijumaa wiki hii, alihojiwa kwa saa tatu mfululizo katika Kituo Kikuu cha
Polisi, Arusha lakini alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba kuachiwa
kwake kunge
hatarisha amani.
hatarisha amani.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kujisalimisha
kwa askari hao usiku huo wa kuamkia juzi, Lema alithibitisha kuwapo kwa
polisi nje ya nyumba yake.
“Wapo nje ya nyumba yangu, wanatishia kupiga
mabomu kama nisipotoka nje, lakini wanajadiliana na walinzi wangu na
mimi nimewataka wanipe hati ya kunikamata,”alisema.
Wakili wa Lema, Humphrey Mtui alisema mahojiano ya
mteja wake na polisi yalidumu kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa 7:50
mchana hadi saa 11:15 jioni, na kwamba walitaka ufafanuzi kwenye hoja
tatu walizodai kwamba zilijengwa kwenye kauli alizotoa Lema wakati
alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA).
Maneno hayo yanayotafsiriwa na polisi kuwa ni
uchochezi ni pamoja na “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni
woga” na “Nimepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa atafika,
asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya
msingi ya kupatiwa ulinzi.”
Kauli nyingine ni “Hawa ndio viongozi wetu
(akimaanisha mkuu wa mkoa), tunaowategemea wanakuja kwenye matatizo
wakijivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off.”
Lema anadaiwa kutamka maneno hayo baada ya Mulongo
kugoma kuzungumza na wanafunzi kisha kurejea ndani ya gari akitaka
viwepo vipaza sauti, kitendo kilichowafanya wanafunzi kuanza kumzomea
kabla polisi kuanza kulipua mabomu ya machozi na kumwondoa eneo la tukio
mkuu huyo wa mkoa.
Lema na Mulongo wote walikwenda IAA kutokana na
tukio la kuuawa kwa kuchomwa kisu kwa aliyekuwa mwanafunzi wa taasisi
hiyo, Henry Kago.
Baada ya vurugu hizo Mulungo alimtuhumu Lema kuandaa mazingira ya yeye kuzomewa.
Wakati hayo yakiendelea, askari katika kituo
anakoshikiliwa Lema jana asubuhi walivutana vikali na ndugu wa mbunge
huyo pamoja na uongozi wa Chadema Mkoa wa Arusha baada ya kumpa dakika
moja kunywa chai aliyoletewa na kukataa asipewe dawa ya meno kutoka kwa
mkewe, Neema.
Habari ambazo gazeti hili lilizipata zinasema
kutokana na hali hiyo, uongozi wa Chadema ulilazimika kumtuma wakili wa
Lema, Method Kimomogoro kwenda Kituo cha Kati cha Polisi Arusha kujua
sababu za polisi kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment