Kwa ufupi
Kocha wa Simba, Patrick Liewig amewataka mashabiki
wa klabu yake wasiwe na mashaka kwani chikukizi wake wana uwezo wa
kuwaadabisha Azam hata Yanga.
http://www.mwananchi.co.tz
KIKOSI CHA SIMBA SC.
DAR ES SALAAM
KOCHA wa Simba, Patrick Liewig amewataka mashabiki wa klabu yake wasiwe na mashaka kwani chikukizi wake wana uwezo wa kuwaadabisha Azam hata Yanga.
KOCHA wa Simba, Patrick Liewig amewataka mashabiki wa klabu yake wasiwe na mashaka kwani chikukizi wake wana uwezo wa kuwaadabisha Azam hata Yanga.
Baadhi ya mashabiki wa Simba wamekuwa na mashaka
na ubora wa kikosi chao kama kina uwezo wa kuzimudu Azam na Yanga na
kupata matokeo mazuri kufuatia msimamo wa Liewig wa kuwatumia zaidi
chipukizi badala ya wachezaji wakongwe.
Simba inayokamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa
Ligi Kuu itashuka dimbani Aprili 13, kuvaana na Azam katika pambano
litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku
ikitarajiwa kuikabili Yanga Mei 18.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam
jana, Liewig alisema haoni sababu ya mashabiki wa klabu hiyo kuwa na
mashaka kwa sababu chipukizi wake wamepevuka vya kutosha na wana uwezo
wa kuikabili timu yoyote kwenye ligi na kupata ushindi.
“Jana (Juzi) tulifanya mazoezi nikiwa na wachezaji
20 tu na wengi wao ni vijana, hakika wana hamu ya mafanikio, wanajituma
na wana morali ya juu,” alisema Liewig.
Alisema “Mechi inayofuata tunacheza na Azam,
naamini kwa kutumia kikosi hiki hiki matokeo mazuri yatapatikana, jambo
la kufurahisha ni kwamba watashirikiana na wachache wenye uzoefu kama
Juma Kaseja na Amri Kiemba ambao ni kama walimu kwao, hakuna sababu ya
kuwa na mashaka,” alisema Liewig.
Alisema kuwa ataendelea na msimamo wa kuwatumia wachezaji vijana kwa vile ndiyo dira hasa ya Simba kufikia mafanikio.
Naye kocha wa Azam, Stewart Hall alisema mawazo
yake kwa sasa ni juu ya mchezo wa Jumatano dhidi ya African Lyon na siyo
Simba wala Yanga.
Hall alisema kwa kuzingatia hatua ligi ilipofikia
hawezi kuipuuza Lyon badala yake atakiandaa kikosi chake kikamilifu kwa
lengo la kuhakikisha kinavuna pointi tatu kwenye mchezo huo.
“Akili na nguvu zangu zote sasa nimezielekeza
kwenye mchezo na African Lyon siku ya Jumatano na siyo hata kwenye Kombe
la Shirikisho Afrika, hauwezi kuwaza jambo la lililoko mbali wakati
kuna lingine lipo karibu na unatakiwa kukabiliana nalo,” alisema Hall.
”African Lyon haiko katika wakati mzuri wakati
huu, inapigana kwa ajili ya kuhakikisha inapata ushindi ikiwezekana
iepuke kushuka daraja, ni mechi ngumu, ni lazima tujiandae kisawasawa.”
Katika pambano la kwanza lililopigwa Oktoba 6, mwaka jana, Azam iliizamisha Lyon bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment