Polisi wa kupambana na ghasia Kenya.
POLISI waonya dhidi ya njama zozote za kuvuruga sherehe za Jumanne za kumwapisha rais wa nne wa Kenya.
Polisi wa Kenya wamewataka baadhi ya watu kuripoti kwa mkuu ya kitengo
cha upelelezi (CID) Nicholas Kamwende kufuatia tuhuma kwamba
wanapanga njama za kuvuruga sherehe za kumwapisha rais mteule, Uhuru Kenyatta
kama rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya siku ya Jumanne.
Inspekta Jenerali wa polisi David Kimaiyo amesema Jumapili kuwa kundi la vijana linapanga maandamano katika maeneo mbalimbali ya Nairobi ambayo hatimaye yatageuka kuwa ghasia wakati wa sherehe hizo za Jumanne.
Kimaiyo ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa polisi wana taarifa kwamba Jeckonia Junga Onyango, aliandaa mkutano na kukamilisha mpango wa njama hizo katika eneo la mabanda la Kibera nje kidogo ya Nairobi.
Taarifa za polisi huko Nairobi zinasema miongoni mwa maeneo yanayopangwa kufanyika maandamano hayo ni pamoja na Kibera, Kangemi, Kamukunji, Dandora na kariobangi.Vijana hao yaripotiwa wamepanga kupora mali kuchoma mali na hata kushambulia wapinzani wao huku wakiwa na silaha kama vile mapanga. Bwana Kimaiyo ameonya kuwa uhalifu wa aina yoyote hutavumiliwa nchini humo.
Habari zaidi zasema waziri mkuu anayeondoka madarakani na ambaye alishindwa katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi uliopita. Raila Odinga amekwenda Afrika Kusini kwa mapumziko.

Taarifa kutoka kwa
msemaji wake Dennis Onyango zinasema .
Odinga hataweza kuhudhuria
sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Uhuru Kenyatta Jumanne licha ya
mwaliko rasmi wa kuhudhuria sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment