Kwa ufupi
Lema anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo akidaiwa
kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya wanafunzi kuchachamaa
kutokana na mauaji ya mwenzao, Henry Kago aliyeuawa kwa kisu karibu na
chuo hicho, Jumanne iliyopita.
http://www.mwananchi.co.tz/Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema.
DAR/MIKOANI.
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema anafikishwa mahakamani leo kwa madai ya kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha, huku ikielezwa kwamba jiji hilo litakuwa katika ulinzi mkali.
Ulinzi umeimarishwa maradufu katika mitaa yote jijini Arusha na Kituo Kikuu cha Polisi anakoshikiliwa mbunge huyo tangu usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita.
Lema anatara
jiwa kufikishwa mahakamani leo akidaiwa kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya wanafunzi kuchachamaa kutokana na mauaji ya mwenzao, Henry Kago aliyeuawa kwa kisu karibu na chuo hicho, Jumanne iliyopita.

Ingawa Jeshi la Polisi linadai ulinzi huo ni
jukumu lao la kawaida la kila siku, lakini wingi wa askari mitaani
umechagizwa na tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani leo kwa Lema
suala linalotokana na rekodi ya wafuasi wa Chadema hasa kukiwa na jambo
linalomhusisha mbunge wao na polisi.
Tangu baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2010,
wafuasi, wapenzi na viongozi wa Chadema Arusha na kitaifa wamekabiliana
mara kadhaa na Polisi mkoani hapa na moja ya matukio yanayokumbukwa ni
lile la maandamano ya Januari 5, 2011 lililoishia kwa mauaji ya watu
wawili huku viongozi kadhaa wa chama hicho wakifunguliwa kesi ya
kusanyiko lisilo halali.
Viongozi wa Chadema wanaokabiliwa na kesi hiyo ni
Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willbrod Slaa, Lema, wabunge
kadhaa na viongozi wa ngazi ya wilaya na mikoa. Polisi kutoka wilaya
jirani na Arusha za Arumeru, Monduli, Karatu na Longido wanahusika
katika ulinzi huo ulioimarishwa tangu juzi.
Wafuasi wa chama hicho kikuu cha upinzani wamekuwa
na desturi ya kujaa mahakamani pale viongozi wao wanaposhtakiwa kwa
kosa lolote na hutoka kwa maandamano yasiyo rasmi kila kesi
inapoahirishwa, jambo ambalo limekuwa likizua mvutano kati yao na polisi
na aghalabu kuishia kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na baadhi kutiwa
mbaroni.
Ulinzi mkali ‘selo’ ya Lema
Polisi wameimarisha ulinzi katika eneo lote la Kituo Kikuu anakoshikiliwa mbunge huyo tangu Ijumaa iliyopita na tangu siku hiyo, watu ambao wamekuwa wakifika hapo kwa sababu mbalimbali wamelazimika kujieleza kwanza kwa askari wa doria kabla ya kuruhusiwa kukaribia lango la kituo hicho.

Katika mitaa mbalimbali nako kuna askari wenye
silaha wanaotembea kwa miguu wakiwa wawiliwawili hadi watatu pamoja wale
wa pikipiki na wa kikosi cha mbwa na farasi.
Kesi nyingine kubwa za leo
Mbali na kesi hiyo, huenda leo Mahakama Kuu ikatoa uamuzi wa maombi ya Jamhuri katika rufani ya kesi ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Jerry Murro na wenzake wawili.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajiwa
kutoa uamuzi wa kama Muro na wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama
‘Dokta’ na Deogratius Mugassa wapandishwe kizimbani tena na kuanza
kusikiliza upya kesi ya rushwa iliyokuwa ikiwakabili au la.
Kesi nyingine ni ya anayedaiwa kumuua Padre Evaristus Mushi ambaye atapandishwa kizimbani kwa mara ya tatu.
Mtuhumiwa huyo, Omar Yusufu Makame, mkazi wa
Mwanakwerekwe, Unguja alikamatwa Machi 29, mwaka huu baada ya uchunguzi
uliofanywa na wapelelezi wa Tanzania walioshirikiana na Shirika la
Upelelezi la Marekani (FBI). Pia leo kesi inayomkabili Mwenyekiti wa
Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba na
wenzake na inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
0 comments:
Post a Comment