Kwa ufupi
Spika wa Bunge, Anne Makinda aliamuru kuondolewa kwa
Bajeti ya Wizara ya Maji, wiki iliyopita na kuitaka Serikali ijipange
upya kwa kushirikiana na Kamati ya Bajeti ya Bunge ili kuangalia namna
ya kuongeza fungu la miradi ya maji. http://www.mwananchi.co.tz/
DODOMA.
WAZIRI wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe anakabiliwa na mtihani mwingine leo atakaporejesha bungeni bajeti yake iliyokwama wiki iliyopita.
Moja ya mtihani mkubwa anaokabiliwa nao ni kulieleza Bunge ikiwa kiasi cha Sh184 bilioni kimepatikana kwa ajili ya kupunguza tatizo la maji vijijini.

Wakati hilo likiendelea, wabunge wa Chadema
waliofukuzwa bungeni wanatarajia kuingia bungeni leo na mmoja wao
Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), anatar
ajiwa kusoma hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
ajiwa kusoma hotuba ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
“Kesho (leo) nitasoma hotuba yangu na nitaifumua
vizuri Serikali hasa kwenye mambo ya migogoro kama wa Loliondo na
masuala ya biashara haramu ya pembe za ndovu kwani ujangili umekithiri
nchini,” alisema Msigwa.
Kwa upande wa Bajeti ya Wizara ya Maji ambayo
ilikwama wiki iliyopita baada ya Profesa Maghembe kuliomba Bunge
kuidhinisha Sh398.3 bilioni ikiwa ni matumizi kwa mwaka 2013/14 lakini
Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji inayosimamia wizara
hiyo, iliomba Bunge kuidhinisha Sh398.3 bilioni na nyongeza ya Sh184.5
bilioni, hoja ya kamati hiyo ilikuwa ni kutaka fedha hizo ziongezwe ili
kupunguza tatizo la maji vijijini ambako ndiko wananchi wanakoteseka
zaidi.
Walitaja baadhi ya maeneo yatakayofanyiwa kazi na
fedha hizo kuwa ni kuendeleza mpango wa upelekaji maji vijijini, kujenga
miundombinu ya kusambaza maji katika vijiji 10 kila halmashauri na
kujenga miundombinu ya kusambaza maji kutoka miradi mikubwa.
“Kamati imebaini kuwa kuna tofauti kubwa kati ya
bajeti inayotengwa kwa ajili ya maji mijini na vijijini, matokeo yake
watu wanaopata majisafi na salama mijini ni asilimia 86 na vijijini
58.6, ikizingatiwa asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini,” inasema
taarifa ya kamati ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi.
Upinzani wataka nyongeza ya Sh500 bilioni
Mwishoni mwa wiki, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema wanataka mpango wa miaka mitano unaojulikana kama ‘Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa’ utengewe fedha za kutosha.
Mwishoni mwa wiki, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema wanataka mpango wa miaka mitano unaojulikana kama ‘Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa’ utengewe fedha za kutosha.
“Kambi inataka kuzingatiwa kwa mpango wa miaka
mitano ambao unataka kutengwa kwa walau Sh500 bilioni za miradi ya kila
mwaka, kwa mwaka huu wizara ikiwa imetenga Sh138 bilioni kwa miradi ya
maendeleo,” alisema Mbowe.
Mpango huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka
mitatu kuanzia 2013/14 mpaka 2015/16. Maji ni miongoni mwa sekta
zilizopewa kipaumbele katika mpango huo unaolenga kuongeza upatikanaji
wa huduma ya maji vijijini.
Kwa mujibu wa hotuba ya Profesa Maghembe, hadi kukamilika kwake, mpango huo utahitaji Sh1.45 trilioni na wananchi milioni 15.4 waishio vijijini watapata maji.
Kwa mujibu wa hotuba ya Profesa Maghembe, hadi kukamilika kwake, mpango huo utahitaji Sh1.45 trilioni na wananchi milioni 15.4 waishio vijijini watapata maji.
Bajeti mpya ya Profesa Maghembe leo itatakiwa
kukata kiu ya wabunge wengi waliotaka kuanzishwa kwa Mfuko wa Maji ili
kuiwezesha Serikali kutokutegemea zaidi fedha za wafadhili.
Hoja ya tano itakayotakiwa kupatiwa majibu na
Profesa Maghembe, ni kumaliza tatizo la bajeti ya wizara yake kutegemea
fedha za wahisani kutokana na mtiririko usioridhisha.
0 comments:
Post a Comment