BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA CHADEMA AILIZA TENA CCM KATIKA MAHAKAMU YA RUFAA.

Kwa ufupi
Uamuzi huo wa kutupilia mbali maombi hayo ulisomwa na Jaji Bernard Luanda, kwa niaba ya jopo la majaji wenzake lililokuwa likiongozwa na Engela Kileo na Salum Massati.
http://www.mwananchi.co.tz 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akionyesha alama ya ‘V’ wakati akitoka Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya rufaa dhidi yake kutupiliwa mbali. Wa pili kulia ni Wakili wake, Tundu Lissu. Picha na Michael Jamson   https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhefXtQKYtxpS_rzaAAAVr0U2UGg6EBl3yTLfp3O475834_57vQ0PFtfmTHbXUEs0dc3EkOGH8VkfDJRVKkUnyxCA8eTLgow7E5BGfwDkTQnB0W4phs9QQkpSIp1dUe7WrrLl1MgmF0OxY/s1600/DSCN3405.JPG 
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akionyesha furaha katika moja ya mikutano ya chama chake.

DAR ES SALAAM. 
MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ameibuka kidedea baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi ya marejeo ya rufaa iliyomrejesha bungeni.
Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na makada watatu wa CCM mkoani Arusha, kupitia kwa Mawakili wao Alute Mughway na Modest Akida wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake hiyo kwa madai kuwa hukumu hiyo haikuwa sahihi.

Hata hivyo, jana Mahakama ya Rufani ilisikiliza maombi hayo kutoka kwa waombaji pamoja na hoja za wajibu maombi na kisha kutupilia mbali maombi hayo ikisema kuwa hayana msingi.
Uamuzi huo wa kutupilia mbali maombi hayo ulisomwa na Jaji Bernard Luanda, kwa niaba ya jopo la majaji wenzake lililokuwa likiongozwa na Engela Kileo na Salum Massati.
Hata hivyo, jopo hilo halikutoa sababu za kutupilia mbali maombi hayo na badala yake lilisema litatoa maelezo ya kina baadaye.
Majaji hao isipokuwa Kileo ndiyo waliosikiliza na kutoa hukumu ya rufaa iliyomrejesha Lema bungeni, ambayo ilikuwa inapingwa na makada hao wa CCM.
Awali, kabla ya kutupilia maombi hayo ya marejeo, mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya waombaji hao kutaka suala hilo lisikilizwe na jopo la majaji saba.
Wakili Mughwai aliwasilisha maombi katika Mahakama ya Rufani akiomba marejeo ya rufaa yahamishwe katika jopo la majaji watatu na kupelekwa kusikilizwa na jopo la majaji saba kwa madai kuwa kuna jambo linatakiwa kushughulikiwa kutokana na mazingira yake.
Wakili wa Lema, Methods Kimomogoro alidai kuwa Wakili Mughwai amechanganya maombi hivyo kuleta utata na kwamba kama alikuwa akitaka yasikilizwe angeyapeleka katika utaratibu ulio sahihi.
“Kanuni ya Nne ya Mahakama ya Rufaa, inasema hakuna kanuni rasmi inayowezesha jopo hili kuhamisha maombi ya marejeo kwenda kwenye jopo la majaji saba kwa ajili ya mapitio,” alisema Kimomogoro na kuongeza:“Labda kama maombi ya mapitio yangekubaliwa, wangekwenda hatua ya pili ya kuomba jopo la majaji saba.
Maombi haya hayajafuata utaratibu hivyo naomba Mahakama iyatupilie mbali kwa kuwa sababu za kisheria hazikidhi na Mahakama haina uwezo wa kuyatolea uamuzi.”
Wakili wa Serikali, Vicent Tangoh alimuunga mkono Kimomogoro na kuongeza kuwa hiyo inaonyesha hakuna maombi yoyote mbele ya Mahakama wala kitu cha kupeleka katika jopo la majaji saba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: