Hilo ni gari alilokuwa akisafiria Padre Alphonce Mhamilawa aliyefariki papohapo baada ya kupata ajali. |
JIMBO Katoliki la Iringa limempoteza Padre Alphonce
Mhamilawa usiku wa kuamkia jana aliyekufa papo hapo kwa ajali ya gari.
Ajali hiyo ilitokea katika maeneo ya Changarawe Mafinga
katika barabara ya Mafina – Makambako ambapo gari iliyosababisha ajali hiyo
ilikimbia.
Kwa mujibu wa mashuhuda walisema kuwa katika maeneo hayo
ajali nyingi zimekuwa zikitokea ambapo magari ya magogo yamekuwa ni chanzo.
Imeelezwa kuwa magari hayo yamekuwa yakifanya kazi usiku
licha ya kuwa hayana taa jambo ambalo ni hatari kwa usalama barabarani.
Hata hivyo mashuhuda walieleza kuwa Padre Mhamilawa aligonga
gari gilo kwa nyuma na kupoteza uhai paleple kutokana na gari lililokuwa
limebeba magogo kutokuwa na taa au alama yoyote na mara baaba ya kusababish
ajali hiyo kukimbia.
Licha ya gari hilo
kukimbia halikuweza kutambuliwa haraka japokuwa gari alilokuwa akisafiria padre
huyo lina namba za usajili T 434 APP.
Mpango wa mazishi unaendelea kufanyika ingawa marehemu
anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Tosamaganga.
HABARI KWA HISANI YA http://gustavchahe.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment