Kwa ufupi
Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika
maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na
gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama
na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na
Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya
muungano.http://www.mwananchi.co.tz
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.Picha na Silvan Kiwale.
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.Picha na Silvan Kiwale.
DAR ES SALAAM.
RAIS Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180.
RAIS Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180.
Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika
maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na
gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama
na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na
Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya
muungano.
Viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu kutoka
Tanzania Bara na Visiwani walishiriki kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni
ishara ya kuuenzi na kuulinda muungano huo.
Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk
Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali,
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim
Seif Sharrif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd.
Wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Rais
mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, Rais mstaafu wa awamu ya pili,
Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Benjamin Mkapa na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa
na Frederick Sumaye.
Baada ya viongozi kuketi katika nafasi zao,
gwaride rasmi lenye gadi kumi lilipita na kutoa heshima zao mbele ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya hapo vijana wa halaiki walionyesha maumbo
mbalimbali kuashiria maendeleo yaliyopatikana nchini kwa muda wa miaka
49 tokea taifa la Tanzania liundwe rasmi kabla ya Wanahalaiki kujipanga
na kuonyesha taswira mbalimbali na kuimba wimbo wa kuhamasisha kudumisha
muungano.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa upinzani hawakuweza kushiriki kwenye maonyesho hayo.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha
NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kumalizika kwa shughuli za maadhimisho hayo, mjumbe wa Kamati Kuu
Chadema ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba, Profesa
Mwesiga Baregu alisema kuwa, Watanzania wanapaswa kujivunia Muungano
walionao kwa sababu umedumu kwa miaka 49.
Aekieleza kuwa ni nadra sana kuona nchi za Afrika au Ulaya kuendeleza muungano wenye umri mkubwa kama huu wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuulinda kuendeleza amani iliyopo.
Aekieleza kuwa ni nadra sana kuona nchi za Afrika au Ulaya kuendeleza muungano wenye umri mkubwa kama huu wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo basi wanapaswa kuuenzi na kuulinda kuendeleza amani iliyopo.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha
kwa wafungwa 4,180 waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza
mbalimbali hapa nchini katika kuadhimisha miaka 49 ya muungano.
Wafungwa waliosamehewa ni wanaotumikia kifungo
kisichozidi miaka mitano, ambapo mpaka siku ya msamaha yaani April 26,
watakuwa wameshatumikia robo ya vifungo vyao, wafungwa wagonjwa wa
Ukimwi, kifua kikuu na kansa ambao wamethibitishwa na jopo la madaktari.
0 comments:
Post a Comment