Rais mstaafu Nelson Mandela.
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ameondoka hospitali baada
ya kulazwa kwa siku 9 na kuzua wasiwasi wa kimataifa juu ya hali yake
ya afya.Taarifa kutoka ofisi ya rais Jacob Zuma imesema rais huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 94 aliruhusiwa kuondoka hospitali Jumamosi baada ya afya yake kuimarika.
Hii ni mara ya tatu kwa mzee Mandela kulazwa hospitali katika muda wa miezi minne. Baada ya kulazwa hospitali Machi 27 mwaka huu rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya mapafu na baadaye nimonia.
Mshindi huyo wa tuzo la amani la Nobeli amekuwa na matatizo ya kupumua tangu alipougua maradhi ya kifua kikuu wakati wa kifungo chake cha miaka 27 jela kwa kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi, wakati wa utawala wa wazungu waliokuwa wachache.
Alikuwa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini mwaka wa 1994 na anaheshimika kote duniani kama mtetezi wa haki na usawa.
0 comments:
Post a Comment