WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI WAKIJIBIRUDISHA KWA KUCHEZA MUZIKI.http://www.mwananchi.co.tz/
SH61 bilioni zimepelekwa kwenye shule za msingi nchini kwa ajili ya uwezeshaji tangu mwaka 2002, imeelezwa.
Fedha hizo ni sawa na Sh7,709 kwa mwanafunzi, sawa na asilimia 77 kwa wanafunzi wote.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina (CCM).
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina (CCM).
Ntukamazina alitaka kujua inakuwaje mpango wa
Serikali katika kutekeleza ahadi ya kuwapatia uwezeshaji (Capitation)
wanafunzi wa shule za msingi kiwango cha Sh10,000 kwa kila mwanafunzi,
kwa ajili ya kununulia vitabu wakati mwingine wanapewa Sh200.
Majaliwa alisema kupitia Mpango wa Maendeleo ya
Elimu ya Msingi , Serikali iliidhinisha kutoa Sh10,000 kwa ajili ya
uendeshaji wa shule kwa kila mwanafunzi.
“Awamu ya kwanza ilitekelezwa mwaka 2002 hadi
2006, awamu ya pili ni mwaka 2007 hadi 2012, Serikali inatekeleza mpango
huo kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo,” alisema Majaliwa.
Kwa Wilaya ya Ngara, alisema zimepelekwa Sh473
milioni ambazo ni Sh6,932 kwa wanafunzi, ambayo nia asilimia 69 kwa
wanafunzi wote.
0 comments:
Post a Comment