Mwaka umepita tangu aliekuwa muigizaji nguli nchini, Steven Charles
Kanumba afariki dunia kwa kifo cha ghafla.
Kanumba atakumbukwa kama mmoja ya wasanii waliofanya
tasnia ya filamu nchini izidi kukua na kupendwa hadi kuteka soko ambalo
kwa kiasi kikubwa lilikuwa likishikiliwa na wasanii wa Nigeria.
Aliondoka wakati bado hajayafaidi mafanikio na kushuhudia namna
mapinduzi aliyofanya yalivyotengeneza ajira kwa vijana wengi,
Pichani ni picha za kumbukumbu zake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
Msanii Lulu akiweka shada la Maua katika kaburi la Steven Kanumba ambapo Lulu kwa sasa yupo nje kwa dhamana kufuatia tukio la kifo cha msanii huyo aliyefariki ghafla mwaka jana.
Sehemu ya matukio ya Waigizaji kwenye kumbukumbu ya Marehemu Kanumba makaburini Kinondoni
Lulu na mama yake mzazi wakiwa katika makaburi ya Kinondoni
0 comments:
Post a Comment