Mlipuko umetokea katika kiwanda cha kutengeza mbolea karibu na Waco,
katika jimbo la Texas nchini Marekani huku idadi kubwa ya watu
wakijeruhiwa na wengine kukwama ndani ya kiwanda hicho
Moshi mkubwa uliokena ukipanda juu kutoka katika eneo la mlipuko. Wazima
moto na magari ya Ambulance pamoja na helikopta sita zilionekana
zikiwasaidia majeruhi.
Wazaima moto hapa wakipambana na moto huo karibu na kiwanda hicho.
Majengo kadhaa yaliharibiwa vibaya mengina yakiwa katika maeneo jirani.
Wazee waliokuwa katika makao jirani ya kuwatunza wazee, walihamishwa
mara moja. Kulikuwa na ripoti kuwa wazima moto walikuwa wanajaribu
kuzima moto wakati mlipuko huo ulipotokea.
Uharibifu mkubwa ulitokea kwa makao ya kuwahifadhi wazee. Mlipuko ulitokea nyakati za usiku.

0 comments:
Post a Comment