Mfanyabiashara Apolnary Malamsha (33) wa Arusha ambaye jicho lake
limepata hitilafu baada ya kutobolewa na chuma cha bomu wiki mbili
zilizopita akiwa Hospitali ya Taifa Muhim
bili jana. Picha na Beatrice Moses.
http://www.mwananchi.co.tz
DAR ES SALAAM.
MFANYABIASHARA Apolnary Malamsha (33) amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuelezwa kuwa chuma cha bomu kilichomtoboa chini ya jicho la kushoto kimeingia ndani na kumharibia mfumo wa kuona.
bili jana. Picha na Beatrice Moses.
http://www.mwananchi.co.tz
DAR ES SALAAM.
MFANYABIASHARA Apolnary Malamsha (33) amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuelezwa kuwa chuma cha bomu kilichomtoboa chini ya jicho la kushoto kimeingia ndani na kumharibia mfumo wa kuona.
Akizungumza kwa masikitiko juzi katika wodi namba
ya 10 Kibasila kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alipolazwa,
Malamsha ambaye ni mkazi wa Olasiti Arusha alisema taarifa hiyo
imemsikitisa na kumuogopesha.
“Nimechunguzwa na daktari ameniambia kwamba
kipande cha chuma kilichotoboa jicho langu kiliingia ndani na kukata
mojawapo ya mishipa inayowezesha jicho kuona kwa hiyo hakuna uwezekano
wa kuona tena,” alisema kwa masikitiko Malamsha.
Malamsha pia anasumbuliwa na kutapika, hali ambayo anadai inachangiwa na vyuma vya mabomu vilivyoingia mwilini mwake.
Naye kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la
Priscus Malamsha ambaye alikuwa akimhudumia alieleza kuhuzunishwa na
habari hizo kwa kuwa inaweza kumpunguzia mdogo wake furaha ya maisha
yake.
“Najisikia vibaya huyu ni mdogo wangu, lakini bomu
limemfanya apoteze furaha yake, tazama anavyotapika kila anachokula,
lakini tutaendelea kumtazama Mungu,” alisema Malamsha ambaye naye ni
mkazi wa Olasiti.
Kijana huyo ni miongoni mwa majeruhi saba
waliofikishwa MNH kwa matibabu zaidi, baada ya kujeruhiwa kwenye mlipuko
wa bomu uliotokea katika Kanisa Katoliki la Mtakafitu Joseph
Mfanyakazi.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa MNH, Jeza Waziri
alieleza kuwa majeruhi karibu wote wanaendelea vyema,baadhi yao
wanaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani kwao hasa kutokana na hali zao
kuendelea kuimarika.
Majeruhi wengine ni Gabriel Godfery (9), Jenipher Joachim (40) na Anastazia Regnard (14).
Wengine ni Albert Njau (35), Faustine Shirima
(33) Fatuma Tarimo (38) ambaye amepimwa na kuonekana ana chembechembe
za vyuma vya bomu ndani ya tumbo lake.
0 comments:
Post a Comment