KATIKA tukio lisilo la
kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali
ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za
watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi
waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Kati
bu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana naKatibu Mkuu wa CDM Ndugu
Slaa.
Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri
kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na
majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na
Uenezi CCM,ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi
wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi
yetu.
Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo,
Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu
wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa
alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja
vibaya kwenye mikutano yake.
Hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze
munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa
watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV
Baada ya tahamaki hiyo,
mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa
kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nahii ni
kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja
hizo...
Tukio hilo linadhihirisha
kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa
CDM hasa Slaa wanao..... Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa
vibaya kupi ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha.
Hali hiyo pia imeonesha
taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa ...
Pia, tukio hilo linaweka
wazi kuwa CDM hawako tayari kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yaliyotokana na
Siasa mbovu za matusi.
Tabia hii ya kukwepa
kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki,
utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni
makosa.
1 comments:
Dk Slaa hakugoma kufanya mjadala na Nape kwa sababu ya kumwogopa. Kwa ufahamu wangu naamini aliona mtego wa kumshushia hadhi kisiasa uliowekwa na CCM kwa kumtuma Nape ambaye kiitifaki siyo size yake.
Kwa tafsiri ya haraka, iwapo Dk Slaa angekubali kushiriki mambo mawili yangejitokeza. Kwanza CCM wangetumia fursa hiyo kumponda kwamba Kinana siyo size yake bali Nape. Pili, Nape angetumia nafasi hiyo kutoa maneno ya kiuenezi (propaganda za majukuani) kumtoa Dk Slaa kwenye hoja za msingi kulinganisha na iwapo Kinana angeshiriki.
Post a Comment